Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia 0712 455 139 au 0687 233 209 wote mnakaribishwa. Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

MAMA TUNU PINDA AOMBA WATU NA MASHIRIKA MBALIMBALI KUSAIDIA KUCHANGIA KATIKA KUENDELEZA ELIMU KWA WATOTO NA VIJANA WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALIBINO)


Mlezi wa chama cha wake wa viongozi Mama Tunu Pinda akipokea vitabu vyenye thamani ya shilngi milioni 35 kutoka kwa Meneja Mkuu wa kituo cha kuendeleza vipaji kwa vijana THT Bwana Mwita Mwaikenda na anaye shuhudia ni Mwenyekiti wa chama cha wake wa viongozi Germina Lukuvi msaada huo wa vitabu ni kwaajili ya kusaidia Elimu kwa watoto na vijana wenye ulemavu wa ngozi (ALIBINO) sherehe hiyo ya makabidhiano imefanyika  katika makazi ya waziri mkuu jijini Dar es salaam.
picha ya pamoja
 Mlezi wa chama cha wake wa viongozi Mama Tunu Pinda (pichani kati) akizungumza na Wanahabari kabla ya ya kupokea vitabu vyenye thamani ya shilngi milioni 35 kutoka kwa Meneja Mkuu wa kituo cha kuendeleza vipaji kwa vijana THT Bwana Mwita Mwaikenda (pichani kulia) na kushoto ni  Mwenyekiti wa chama cha wake wa viongozi Germina Lukuvi ..
THT yatoa vitabu kwa maktaba ya walemavu wa ngozi Kanda ya Ziwa
Nyumba ya vipaji Tanzania (THT) imetoa vitabu vya Sayansi, Sanaa na Hesabu kwa maktaba ya walemavu wa ngozi inayotarajiwa kujengwa na taasisi isiyo ya Kiserikali ya New Millennium Group.

Vitabu hivyo vyenye thamani ya jumla ya shilingi milioni 35 vimetolewa kwa lengo la kusaidia kukuza elimu Tanzania hasa kwa jamii ya walemavu wa ngozi, ikiwa ni mchango wa THT kwa huduma za jamii.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Meneja Mkuu wa Nyumba ya Vipaji Tanzania, Mwita Mwaikenda alisema taasisi yake iliona changamoto ya vitabu baada ya taasisi ya New Millennium Group kutembelea vituo vya maalbino vya kanda ya ziwa mwanzoni mwa mwaka huu.

‘Msaada huu wa vitabu sisi kama THT tumeutoa ili kuiwezesha maktaba ya walemavu kupata vitabu vya kujisomea na hivyo kujiongezea maarifa baina yao’ alisema Mwita. Kwa upande wake Mlezi wa Taasisi ya New Millenium Group, Mama Tunu Pinda, alisema wanaishukuru THT kwa msaada huo ambao alisema ni muhimu sana kwa ajili ya lengo lao la kusaidia kuiwezesha kielimu jamii ya watoto wenye ulemavu wa ngozi.

‘Hakika msaada huu utasaidia kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha lengo la kuanzisha maktaba kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi, na tunaaamini msaada huu utawapa changamoto wadau wengine kusaidia kukamilisha maktaba hii ya kwanza kabisa kuhudumia watu wenye ulemavu wa ngozi’ alisema Mama Pinda.


Naye Mwenyekiti wa New Millennium Group, Mama Germina Lukuvi anasema pamoja na vituo hivyo kuwa na sehemu ya malazi kwa maalbino bado kumekuwa na changamoto ya sehemu za kujisomea na New Millennium Group itaendelea kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...