Meneja
Msaidizi Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Anita Goshashy (Watatu
Kushoto) akikabidhi magodoro kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya
Mwananyamala, Dkt. Sophinias Ngonyani (Kushoto). Wakishuhudia ni
Wafanyakazi wa Benki ya Exim. Benki
ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wadi ya Wazazi katika Hospitali ya
Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika
kuadhimisha Siku ya Mama Duniani. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Meneja Msaidizi Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Anita Goshashy (Wakwanza Kushoto) na
Meneja Msaidizi Msoko mwenzake Bi Violet Bikoche (Wapili Kushoto)
wakizungumza na mmoja kati ya kinamama waliojifungua mara baada ya
kukabidhi magodoro katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala. Benki
ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wodi ya Wazazi Hospitalini hapo
mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani
Meneja
Msaidizi Masoko wa Benki ya Exim Tanzania, Bi Anita Goshashy (Watatu
Kushoto) akikabidhi magodoro kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya
Mwananyamala, Dkt. Sophinias Ngonyani (Kushoto). Wakishuhudia ni
Wafanyakazi wa Benki ya Exim. Benki
ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wadi ya Wazazi katika Hospitali ya
Rufaa ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki katika
kuadhimisha Siku ya Mama Duniani.
Katibu
wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim Bi. Erica Mbutu (wakwanza
kushoto) na Meneja Msaidizi Msoko wa Benki ya Exim, Bi Violet Bikoche
(Wapili Kushoto) wakizungumza na mmoja kati ya kinamama waliojifungua
mara baada ya kukabidhi magodoro katika Hospitali ya Rufaa ya
Mwananyamala. Benki
ya Exim imetoa magodoro 60 katika Wodi ya Wazazi Hospitalini hapo
mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya Mama Duniani.
Muuguzi
Kiongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mwananyamala Sr. Tuswege Mwamwaja (wa
kwanza kulia) akifafanua jambo kwa wafanyakazi wa Benki ya Exim
Tanzania mara baada ya Benki hiyo kukabidhi magodoro 60 katika Wodi ya
Wazazi Hospitalini hapo mwishoni mwa wiki katika kuadhimisha Siku ya
Mama Duniani.
===== ===== ======
BENKI ya Exim ya Tanzania imeadhimisha Sikukuu ya Mama Duniani kwa kuchangia magodoro 60 katika wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mwananyamala iliyopo jijini Dar es Salaam katika kutoa heshima kwa kinamama wote na kuunga mkono jitihada za kuboresha afya ya uzazi nchini.
BENKI ya Exim ya Tanzania imeadhimisha Sikukuu ya Mama Duniani kwa kuchangia magodoro 60 katika wodi ya wazazi ya Hospitali ya Mwananyamala iliyopo jijini Dar es Salaam katika kutoa heshima kwa kinamama wote na kuunga mkono jitihada za kuboresha afya ya uzazi nchini.
Kwa sasa, Hospitali ya Mwananyamala
ambayo ni hospitali kubwa ya rufaa jijini Dar es Salaam inatoa huduma kwa
wakinamama wanaotarajia kujifungua zaidi ya 3100 kwa mwezi, ikiwa na vitanda
136 tu katika wodi hiyo ya wazazi.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magodoro hayo
hospitali hapo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Meneja Msaidizi Masoko
Bi Anita Goshashy alisema mchango huo ni moja kati ya utekelezaji wa shughuli
za benki yake zinazolenga kuisaidia jamii inayoizunguka.
“Mwaka jana, Benki ya Exim imeweza kufikia faida
ya shilingi bilioni 20, na tumekuwa na utamaduni wa kurejesha kile tukipatacho
toka kwa jamii. Sasa, leo hii tuko hapa Mwananyamala kukabidhi vitu hivi, ikiwa
kama njia ya kutambua mchango wa kina mama zetu na kuonyesha jinsi gani
tunaisaidia jamii inayotuzunguka kama benki,” alisema Bi. Goshashy, aliongeza
kuwa benki itaendelea kuipiga jeki jamii hususani katika sekta ya Afya,
Mazingira na Elimu.
Bi. Goshashy alisisitiza kuwa, “Leo hii tunakabidhi
magodoro haya ili kuweza kusaidia kuboresha uzazi uliosalama. Kina mama wengi
wanaotarajia kujigfungua ufariki wakati wakijifungua. Mchango wetu leo
utasaidia katika katika kuboresha hali hiyo hapa Hospitali ya Rufaa ya
Mwananyamala.
Jitihada zetu hazitaishia hapa tutaendelea kufanyakazi
karibu na jamii inayotuzunguka.” Naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Mwananyamala, Dkt. Sophinias Ngonyani aliipongeza Benki ya Exim kwa msaada huo,
na kuongeza kuwa msaada umewafikia kwa wakati muafaka na kuziasa taasisi
nyingine za kifedha na makampuni mengine nchini kuiga mfano huo.
“Kwa niaba ya Jamii ya Hospitali ya Mwananyamala,
Ningependa kuelezea shukrani zangu za dhati kwa hatua nzuri mliyoichukua kuweza
kutusaidia vitanda hivi ambavyo vitatumika kwa wakinamama ambao tunawathamini
kwa kiasi kikubwa maishani mwetu. Mchango huu utasaidia Jamii ya Mwananyamala
kwa kiaasi kikubwa sana,” alisema Dkt. Ngonyani.
Dkt Ngonyani alisema kuwa kadri ya serikali
inapojitahidi kuzipatia vifaa vituo vya afya, jitihada haziwezi kutoshereza
mahitaji yote kwa ujumla katika hospitali hizi, ndiyo maana kuna haja ya wadau
wengine, hususani makampuni kujitokeza na kuunga mkono jitihada hizo na kuweza
kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya afya nchini.
No comments:
Post a Comment