Zikiwa
zimesalia takribani siku 34 kuweza kuanza rasmi kwa michuano ya kombe
la Dunia, polisi nchini Brazil wamefanya mgomo wa saa 24 Jumatano
iliyopita katika miji kadhaa nchini humo ukiwemo mji mkuu wa ‘Rio De
Janeiro’ ambao utaandaa mechi saba ikiwemo fainali ya kombe hilo
itakayochezwa Julai 13 wakidai mazingira bora ya utendaji kazi.
Shirikisho hilo la polisi limefanya maandamano ya amani huku
msemaji wa jeshi hilo Renato Deslandes akinukuliwa na BBC akisema kwamba
Polisi wataendelea na mgomo katika kipindi cha wiki za mbeleni ambapo
michuano hiyo itakuwa tayari imeshaanza kutimua vumbi endapo kama
serikali haitaongeza kuwalipa kulingana na mfumo wa bei ulivyo kwa hivi
sasa.
Aliendelea kusema kuwa mishahara wanayolipwa hivi sasa
inacheza kati ya dola za kimarekani 3,200 mpaka 5800 kabla ya kukatwa
kwa kodi na ulinzi jamii na kuongezea kwamba tangu kutokea kwa mfumo wa
bei mishahara yao haikuweza kupandishwa.
Wakati hayo yakiendelea, kocha mkuu wa Brazil ambao ni
wenyeji wa michuano hiyo ‘Luiz Filipe Scolari’ amekizindua kikosi chake
kitakachoshiriki kwenye kinyang’anyiro hicho huku akiweka wazi majina ya
wachezaji 23 watakaoiwakilisha nchi hiyo katika fainali za Dunia mwaka
huu.
No comments:
Post a Comment