Hitmaker
wa ‘Whip My Hair’ Willow Smith(14) ambaye ni binti wa muigizaji nguli
Will Smith amezua maswali mengi kwa mashabiki na wapenzi wa muziki wake
kufuatia picha alizopiga akiwa kitandani na njemba wakiwa vifua wazi
kuzagaa kama njugu kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
Mwimbaji huyo kinda alipigwa picha hiyo akiwa kitandani na
staa wa filamu aitwae Moises Arias(20) AKA ‘Hanna Montana’ kipindi cha
mapumziko ya Tamasha la muziki na sanaa ‘Coachella ambalo hufanyika
kila mwaka mjini Los Angels Marekani.
Hata hivyo wazazi wa Willow
hawakuonyesha kabisa kushtushwa na kitendo hicho zaidi ya mama mzazi wa
binti huyo ‘Jada Pinkett’ kuvitupia lawama vyombo vya habari kwa kukuza
jambo huku akidai kwamba hakuna kitu kilichokuwa kikiendelea baina ya
binti yake na staa huyo wa filamu.
Pichani ni Willow Smith akiwa amejiachia kwa raha zake na njemba ‘Hannah Montana’
No comments:
Post a Comment