Kampeni
ya #bringBackOurGirls imeonekena kugusa hisia za watu wengi hali
iliyopelekea kuungwa mkono na watu mbalimbali mashuhuri hasa wale
wanaojua uchungu wa mwana akiwemo mke wa Rais wa Marekani Michelle
Obama, pamoja na wanamuziki kama vile LudaCris, John Legend, Naomi Campbell, Jamie Foxy, Drake, Justine TimberLake, Alicia Keys, 2Face na wengine kibao.
Kwa huzuni kabisa, mastaa waliotajwa hapo juu waliweza
kuweka ujumbe kwenye akaunti na kurasa wanazomiliki za kwenye mitandao
ya kijamii wakitaka kuachiliwa huru kwa wanafunzi wa kike 234 wa shule
ya bweni ya Chibok ambao waliotekwa na wanamgambo wa kundi la Boko Haram
yapata wiki mbili zilizopita katika jimbo la Borno nchini Nigeria.
”Our prayers are with the missing Nigerian girls and their families. It’s time to #BringBackOurGirls.” aliandika mke wa Rais wa sasa wa marekani Bi.Michelle Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter .
Alicia Keys
Justin TimberLake
2Face Idibia
Mastaa
mbalimbali wakiwa na mbango yaliyobeba ujumbe mzito wa ”Real Men Don’t
Buy Girls” ikiwa ni katika kupinga kitendo kinachofanywa na Boko Haram
cha kuwashikilia wasichana hao na kutaka kuwauza kwa watu wa mataifa
mengine .
No comments:
Post a Comment