Wakuu
wa tume ya uchaguzi nchini Afrika-Kusini wametangaza kuwa shughuli ya
kuhesabu kura inaenelekea kukamilika baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika
juzi kwa mara ya tano tangu utawala wa mwafrika mzungu.
Chama tawala cha ANC kinaongoza kwa zaidi ya asilimia 63, huku kile cha Democratic Alliance kikiwa na asilimia 23.
Chama kipya cha Economic Freedom Fighters cha Julius Malema kikiwa katika nafasi ya tatu.
Jumla ya asilimia 96 ya kura zilizopigwa zimehesabiwa.
Mwandishi
wa BBC Andrew Harding anasema kuwa ukosefu wa ajira,ufisadi na ukosefu
wa usawa katika jamii ni changamoto kubwa lakini wapiga kura bado wana
imani na chama cha African National Congress ANC.
Tume
ya uchaguzi imesema kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani katika maeneo
mengi ya nchi huku asilimia 73 ya wapiga kura wakijitokeza kupiga kura.
Uchaguzi
huu ni wa kwanza tangu nchi hiyo kuondokewa na rais wa kwanza mzalendo
wa nchi hiyo hayati Nelson Mandela. Afrika Kusini imetimiza miaka 20
tangu kumalizika kwa utawala wa wazungu.
Idadi kubwa ya wananchi imekuwa ikilalamikia utenda kazi wa serikali hasa kwa kuwa kuna kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira.
Wadadisi
wanasema kuwa chama cha ANC huenda kikatumia fursa hii kuimarisha
uchumi wa nchi hasa baada ya miaka mitano ya kile kinachosemekana kuwa
utawala mbovu wa Rais Jacob Zuma.
-BBC
No comments:
Post a Comment