Rapa na Mtayarishaji wa muziki ‘Andre Romelle Young’ maarufu kwa jina la steji Dr.Dre
amesema kuwa yeye ni bilionea wa kwanza katika Hip Hop kufuatia
kampuni ya Apple kutangaza kuinunua kampuni yake ya Beats Electronics
inayotengeneza Headphones za Beats by Dre.
”Bilionea wa kwanza katika Hip Hop kutoka West Coast (alafu akatia na kionjo cha tusi)” alisema Dre katika video fupi aliyochukulia na staa wa filamu za fast & Furious muigizaji Tyrese Gibson.
Katika Video hiyo Tyrese alikuwa akijadili kuhusiana na
orodha iliyotolewa na jarida la Forbes ya wasanii wa Hip hop wanaoongoza
kwa kuwa na mkwanja mrefu.
”Haiwezekani” Tyrese anasema orodha ya Forbes imebadilika ghafla” ”kwa hatua kubwa” aliongezea Dre.
Kama ilivyoripotiwa hapo jana(May08) na mtandao wa gizmodo
uliosema kwamba Apple imepanga kuinunua Beats Electronics inayomilikiwa
na Dre pamoja na Jimmy Iovine kwa gharama ya dola za kimarekani Bilioni 3.2 huku dola bilioni 1 zikitajwa kuingia mfukoni mwa mtayarishaji huyo..
Kwa mujibu wa kituo cha utangazaji cha CNBC walisema kwamba
ununuzi huo unakwenda kinyume na sera za muanzilishi wa kapuni hiyo
Steven Jobs aliyefariki Dunia mwaka 2011, zilizokuwa zikipinga ununuzi
wa vitu vyenye gharama kubwa.
Dre anayeshikilia nafasi ya pili hivi sasa kwa wasanii wa Hip
Hop wenye hela ndefu huku utajiri wake ukitajwa kufikia dola milioni
550 akiwa amemzidi Jay Z kwa tofauti ya dola milioni 30. Hiyo ni kwa
mujibu wa orodha iliyotolewa na jarida la Forbes…
“I don’t really care about any of that,” “Jay Z is my guy, man. I love him to death.” alisema Dr.Dre baada ya kupigwa swali na muandishi kuhusiana na anavyojisikia kuwa juu ya Jay Z
Tazama Video fupi hapo chini umsikilize alichosema Dre baada ya kupata shavu hilo
No comments:
Post a Comment