Mshindi wa Tuzo ya Oscar, mwigizaji mwenye asili ya Kenya
‘Lupita Nyong’o’ ameweza kupata nafasi ya kupiga stori mbili tatu kwa
lugha ya kiswahili na Rais wa Marekani ‘Barack Obama’ baada ya kupata mualiko rasmi wa chakula cha jioni kutoka katika ikulu ya Marekani maarufu kama White House.
Lupita akiwa ameongozana na mama yake mpendwa, waliweza
kukutana na Mr.prezidenti pamoja na mkewe Bi.Michelle Obama huku wawili
hao wenye asili ya Kenya wakiripotiwa kuzungumza Lugha ya Kiswahili
katika maongezi yao hayo.
Kwa hivi sasa Lupita ni balozi wa vipodozi vya Lancome huku
akitajwa kuwa miongoni mwa mastaa daraja la kwanza Dunia akiwa na
utajiri unaokadiriwa kufikia dola za kimarekani milioni 43 ukichangiwa
zaidi na mauzo ya filamu aliyochezwa ya 12 years a slave.
Katika Tukio lingine, Lupita
aliweza pia kula bata sambamba na Malkia wa muziki ‘Beyonce Knowles’
kwenye after party ya Met Gala
No comments:
Post a Comment