Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia 0712 455 139 au 0687 233 209 wote mnakaribishwa. Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Anti-Virus mixtape ni gumzo kitaani
Anti-Virus mixtape imenena On June 30, 2010, in Print, Swahili, by bahati ..Mixtape hii imeibua hoja kadhaa,
 Dawa ya virusi ndio imeshamwagwa mtaani, na parapanda ndio imeshalia. Msanii wa muda mrefu, Sugu ndio ameshapakua ile mixtape yake ya AntiVirus niliyolonga juu yake kitambo kidogo. Mixtape hii imeleta mshikemshike jijini na sitashangaa kama pia imeleta kizunguzungu kwenye jamii ya wana bongo flava.
Nyimbo ya I Wanna Kill Ru.., unaopatikana kwenye mixtape hiyo umepelekea Sugu kuitwa na kuhojiwa na polisi. Pamoja na mistari ya nyimbo hiyo kuwa mikali kidogo, lakini je, ni kweli kuwa Sugu anataka kuua au ni utundu tu wa mashairi?
Mixtape hii imeibua hoja kadhaa, moja ikiwa ya uhusiano kati ya redio na wasanii, pamoja na nafasi ya redio katika kukuza sanaa nahata nafasi ya redio kuuwa sanaa. Neno bongo flava lilizaliwa redioni, na redioni huko huko ndipo bongo flava ilipolelewa na kukuwa mpaka hapa ilipofikia. Lakini je, redio zimefanya kazi ya kutosha kukuza ubunifu katika sanaa hii ya bongo flava? Kwani, swala la ma-Dj kuwa mameneja wa wasanii linapigiwa kelele kila siku, kwani ma-dj hao mamaeneja wanashukiwa kuwapendelea wasanii wao. Kama hii ni kweli, upendeleo huo ni ufa, tena ni ufa unaoweza kuhatarisha maendeleo ya sanaa hii inayoajiri vijana wengi.
Pamoja na yote, mashairi ya Sugu na wenzake katika mixtape hii yanaweza kuangaliwa katika pande mbili. Pande ya kwanza, ni kuwa mashairi yao yanachochea chuki na hata kuleta fujo. Pande ya pili, ni kuwa mashairi yao yanaongea ukweli mtupu, na lugha kali waliyotumia ni kutokana na kuchoshwa na unyonyaji katika sanaa ya bongo flava. Inawezekana pia Sugu ameamua kujitoa muhanga na kutuonesha roho ya udhubutu, kwani Watanzania tuna sifa ya kukubali yaishe. Sasa basi, kama mashairi ya mixtape hii yataleta fujo, Sugu na wenzake watakuwa na kesi ya kujibu. Lakini kama tunakubaliana kuwa mabadiliko “changes” huja mara nyingi kutokana na mapambano ya aina fulani, basi Sugu ndio anatuonesha njia, kama Bob Marley alivyoimba Get Up Stand Up.
Swali, je Mixtape ya Antivirus inatetea muziki wa bongo flava dhidi ya wachache wanaouyumbisha au inataka kuchochea fujo zinazotokana na chuki kibinafsi? Sasa soma tamko rasmi alilotoa Sugu kwa vyombo vya habari juu ya kasheshe zilizomkumba siku mbili hizi tangia Mixtape ifike mtaani

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...