Msanii nguli wa muziki Tanzania, Rehema Chalamila maarufu
kama Ray C au kiuno bila mfupa amelazwa katika hospitali ya Mwananyamala
iliyopo wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam akisumbuliwa na
ugonjwa wa Dengue ambao umepata umaarufu wa ghafla na kuwa ndio habari
ya mjini kwa hivi sasa hasa kutokana na kuambukiza idadi kubwa ya wakazi
waishio jijini Dar es salaam huku dalili zake zikitajwa kufanana na
zile za Malaria.
“Tumemfanyia vipimo, ana homa kali sana lakini hana malaria.
Baada ya kuchunguza dalili, tumechukua vipimo na kubaini kwamba amepata
maambukizi ya dengue, hivyo tunaendelea kumpa matibabu kwa sasa,” alisema
daktari mmoja aliyekuwa zamu ambaye hakupenda kutaja jina lake, wakati
akimweleza mwandishi wa habari wa gazeti la Mwanaspoti kuhusiana na hali
ya mwanamuziki huyo.
Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na madaktari mbalimbali,
wanaielezea Dengue kama ugonjwa unaosambazwa na mbu mweusi aina ya
Aedes Egypitia ambaye hueneza virusi vya ugonjwa huo hasa majira ya
asubuhi na jioni.
No comments:
Post a Comment