Aliyekua Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Ananilea Nkya
----
Dr Kitila, Mwigamba na mwanangu Zitto,
Niwape ushauri kidogo.
Kama
kweli haya tuliyoelezwa mmehusika, ni vema mkakubali kwamba kuna mahala
mmepotoka kiasi. Sisi tunatambua kuwa binadamu huweza kukosea ili mradi
mtu asifanye makosa kwa kukusudia. Adhabu iliyotolewa kwenu
kuvuliwa vyeo, nionavyo mimi utaratibu wa kibinadamu wa
kurekebishana.Kama kweli mnahusika kwa chembe katika haya, na kama
kweli
hamjanunuliwa kuvuruga nia njema ya kujenga upinzani imara wa kisiasa
nchini kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya wananchi na nchi kwa
ujumla, basi msiwe na papara.
Tulieni tafakarini na kisha ombeni radhi.
Ninaamini mkifanya hivyo, uongozi wa chama chenu,wanachama na
Watanzania watawasamehe na kisha rudini kazini jengeni chama chenu
kiweze kuimarika zaidi kwa ajili ya kuwatumikia
Watanzania kwa umakini, uaminifu na ujasiri usiotiliwa shaka.
Mkifanya
hivyo mtajenga utaduni mpya wa kuigwa nchini na wanasiasana heshima
yenu itapanda juu. Mkifanya vinginevyo, mnaweza mkaonekana mliingia
CHADEMA kwa lengo la kuvuruga au kutafuta umaarufu, fedha au
vyeo haraka haraka.
Mungu awabariki.
Ananilea Nkya
E-mail:ananilea_nkya@yahoo. com
E-mail:ananilea_nkya@yahoo.
No comments:
Post a Comment