Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Mh. Freeman
Mbowe (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo
pichani) waliofika kwenye Makao Makuu ya Chama hicho leo,ambapo Kamati
ya Chama hicho imeamua imeamua kuwavua nyadhifa mbali mbali baadhi ya
viongozi wa Juu wa Chama hicho akiwepo Mh. Zitto Kabwe. Wengine pichani
toka kushoto kwake ni Mwenyekiti wa Udhamini wa Chama hicho, Sylvester
Kanyansi Masinde, Katibu Mkuu, Dk Wilbroad Slaa, Mwanasheria Mkuu wa
Chama, Tundu Lisu na viongozi wengine wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
Na Chadema Blog
KAMATI
kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA imewavua Uongozi
Viongozi wake watatu baada ya Kugundua waraka wa Siri uliowahusisha na
mpango wa kukipasua Chama vipande vipande.
Viongozi
waliovuliwa Uongozi ni Zitto Kabwe ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Dr
Kitila Mkumbo na Samsoni Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda ya
Kaskazini. Hatua hiyo ilichukuliwa katika kikao cha kamati kuu
kilichokuwa kimefanyika kwa siku mbili katika Ukumbi wa Ubungo Plaza,
Dar es Salaam.
Akizungumza
katika Mkutano na Waandishi wa Habari Mh Tundu Lissu amesema katika
Waraka huo kulikuwa na mtu anayejulikana kama MM ambaye ni Naibu Katibu
mkuu Zitto Kabwe, M1 ni Dr Kitila Mkumbo, M3 ni Samsoni Mwigamba na M2
hajajulikana ambaye ni mtumishi wa makao makuu ya Chadema. Mh Lissu
amesema Dr Kitila Mkumbo alikana kabisa kumfahamu M2.
Mh
Tundu Lissu amesema Waraka huo uliojulikana kama Waraka wa Ushindi
unavunja katiba ya Chama kwa sababu umepandikiza chuki za kidini,
majungu na kukashifu viongozi wa Chama kinyume na katiba ya CHADEMA.
Mh
Tundu Lissu amesema tuhuma zote zilizoko katika waraka huo hazijawahi
kuwasilishwa kwenye kikao chochote halali cha chama kinyume na matakwa
na masharti ya katiba yetu. Mh Tundu Lissu Amesema Kamati Kuu imeamua
kuwavua nyadhifa zao zote watu wote waliotajwa katika waraka huo ambao
ni Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba.
Pia
kamati kuu imeunda kamati ya kuchunguza na kufuatilia mhusika mwingine
M2 ambaye anadaiwa ni Mtumishi wa Makao Makuu ili hatua stahiki ziweze
kuchukuliwa dhidi yake.
Kamati
Kuu imeagiza wahusika wote waandikiwe barua za kujieleza ni kwanini
wasivuliwe uanachama kwa makosa hayo makubwa waliyofanya.
Pia Kamati Kuu imeagiza mchakato wa kumvua Zitto nafasi yake ya Unaibu wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Lissu
amesema Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe na Dr. Kitila Mkumbo waliomba
kujiuzulu nyadhifa zao zote baada ya waraka wao kukamatwa lakini Kamati
Kuu iliwakatilia baada ya kuona kuwa kukubaliana na maombi yao hayo
ilikuwa ni kama kuwaacha wajiuzulu kwa heshima ambayo hawaistahili hata
kidogo.
Wakati huo huo kamati kuu imemteua Mh Tundu Lissu kuwa Mwanasheria mkuu wa Chama.
No comments:
Post a Comment