Kila tarehe 16 November ni siku ya
kuzaliwa kwa Albert Mangweha a.k.a Ngwea ambae alizaliwa Mbeya mwaka
1982 na baadae wazazi ambao ni wenyeji wa Songea walihamia Morogoro.
Shughuli ya kukumbuka siku yake ya
kuzaliwa imeambatana na siku ya kuhitimisha msiba yaani 40 na
ilifanyika nyumbani kwao kihonda mkoani Morogoro kwa kuandaa misa ya
kumuombea ambayo ilianza na mkesha wa tarehe 15 kuamkia 16.
Hizi ni picha za kuanzia usiku wa mkesha nyumbani kwao Albert mpaka kanisani.
Hii ni kwaya ikiimba nyimbo za maombolezo nyumbani.
Miongoni mwa waliohudhuria ni pamoja na Bdozen toka XXL ya Cloudsfm,Young Dee na Dj venture aliyewahi kuwa meneja wa Ngwea.
Asubuhi kulipokucha tulielekea
kanisani barabara ya kuelekea Dodoma ( Mtakatifu Monica parokia ya
Kihonda) ambapo misa ilianza sa 1 asubuhi na iliongozwa na paroko wa
kanisa hilo Padri Octavian Msimbe.
Misa ilipokamilika waumini wote
walisogea mpaka Makaburini alipolala Ngwea ambapo ni karibu na kaburi la
baba mzazi wa Albert, mzee Keneth Mangweha na baadae ibada ikahamia
alipolala rapper Albert Mangweha.
Hili hapa juu ni kaburi la mzee Mangweha.
Misa ikiendelea kwenye kaburi la Ngwea.
Misa ilipoisha watu wengi waliokua
karibu wapendwa wa ALBERT hawakuondoka mapema makaburini ambapo ndugu
na mama mzazi walitangulia nyumbani lakini wengine waliendelea kuwa
makaburini wakiwasha mishumaa.
Kutoka kushoto ni M2the p,Dark
Master,Quick Rocker,Dj Venture na Dulah Spatan na kulia ni Bdozen,Geez
Mabovu na ndugu waliokua karibu na Ngwair wakisali kwenye kaburi.
Mama mzazi wa Marehemu Ngwea akiweka shada la maua kwenye kaburi la NGWEA.
Bdozen akiwasha mshumaa.
Young Dee nae akiwasha mshumaa juu ya kaburi la NGWEA.
Dark Master akipiga saluti kwenye kaburi la Ngwea.
Baada ya kuwasha mishumaa na kuweka
mashada ya maua zilisikika nyimbo za Marehemu Ngwea ambazo zilikua
zikipigwa kutoka kwa gari ya producer Maneck zikiwa ni nyimbo za Ngwea
ambazo hazikuwahi kutoka lakini zilikua studio ambapo waliokuwemo eneo
hilo wakati zikipigwa ni pamoja na Quick Rocker, Maneck,Bdozen,Young
Dee,Dark master,Geez mabovu,Dj ventureDulah spatan, Muro Junior aliyekua
meneja wa Ngwea hadi kipindi cha mwisho pamoja na Jordan ambae ni mmoja
ya wadogo wa Ngwea kimuziki aliakua akisimamiwa kimuziki na Ngwea.
Hapa ni nyumbani kwa kina Albert Mangweha.
Muziki wa taratibu pamoja na nyimbo za Ngwea zilikua zikiendelea kusikika.
R.I.P Ngwea.
Picha ==>> Milardayo.com
No comments:
Post a Comment