Airtel, Rotary club, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mr.Price, Home Shopping Center- waungana kuendesha kampeni za Usalama Barabarani kupitia MPINGA CUP
Meneja Uhusiano wa
Airtel bw Jackson Mmbando akiongea wakati wa kutangaza kuanza kwa
mashindano na kukabidhi vifaa vitakavyotumika katika mashindano yatakayo
shirikisha waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda yanayoitwa “
mpinga Cup” yenye lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa
madereva wa bodabora jijini Dar es Saalam . katikati ni Mkuu wa kikosi
cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga, akifatiwa na mwakilishi wa
Meneja Uendeshaji Home Shopping center Yahaya Zuludi na Mwakilishi wa
Rotary club Dar es Saalam Vinay Choudary ambao pia ni wadhamini wa
michuano hiyo. makabidhiano yamefanyika leo katika ofisi kuu ya trafiki
Dar es salaam
Meneja Uhusiano wa
Airtel bw Jackson Mmbando akimkabidhi Mkuu wa kikosi cha Usalama
barabarani SACP. Mohamed Mpinga jezi zitakazotumika katika michuano ya
mpinga cup itakayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda
yenye lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani ili kupunguza idadi ya
ajali za barabarani . michuano ya hiyo pia imedhaminiwa na Rotary Dar
es Saalm, Home shopping center pamoja na Mr Price na itafanyika kwa
muda wa wiki nzima, wakishuhudia katikati ni Meneja uendeshaji Home
shopping center Yahaya Zuludi na kulia Mwakilishi wa Mr. Price Sudhirm
Maharaj.makabidhiano yamefanyika leo katika ofisi kuu ya trafiki Dar es
salaam
Meneja Uhusiano wa
Airtel bw Jackson Mmbando akimkabidhi Mkuu wa kikosi cha Usalama
barabarani SACP. Mohamed Mpinga mipira itakayotumika katika michuano ya
mpinga cup itakayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda
yenye lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani . wadhamini wengine wa
Mping cup ni pamoja na Rotary Dar es Saalm, Home shopping center pamoja
na Mr Price . wakishuhudia katikati ni Meneja uendeshaji Home shopping
center Yahaya Zuludi na kulia Mwakilishi wa Mr. Price Sudhirm Maharaj.
makabidhiano yamefanyika leo katika ofisi kuu ya trafiki Dar es salaam
Mkuu
wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga akionyesha jezi zitakazotumika
katika michuano ya mpinga cup itakayoshirikisha waendesha
pikipiki maarufu kama Bodaboda.
Mwakilishi
wa Mr Price Sudhirm Maharaj akikabidhi jezi kwa Mkuu wa kikosi cha
Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga zitakazotumika katika michuano
ya mpinga cup itakayoshirikisha waendesha pikipiki maarufu kama
Bodaboda yenye lengo la kutoa elimu ya usalama barabarani . michuano ya
hiyo pia imedhaminiwa na Airtel, Rotary Dar es Saalm, Home shopping
center pamoja na Mr Price.
PRESS RELEASE:
UDHAMINI WA MASHINDANO YA BODABODA –‘‘MPINGA CUP’’
Airtel,
Rotary club, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mr.Price, Home
Shopping Center- waungana kuendesha kampeni za Usalama Barabarani
kupitia MPINGA CUP
Wadhamini mashindano ya mpira wa
Miguu kwa waendesha bodaboda kwa lengo la kutoa elimu ya usalama
barabarani .Wakabidhi vifaa vya michezo vikiwemo Mipira, jezi, fulana
pamoja na zawadi ya mshindi
Dar es salaam Airtel kwa kushirikia na Rotary club, Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mr.Price, Home Shopping Center pamoja
na Jeshi la polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani imeibuka na
mpango wa kipekee kupitia mchezo wa mpira wa miguu kwa madereva wa
bodaboda utakaowakutanisha pamoja waendesha boda boda wa jijini Dar es
salaam ili kuimarisha uelewa wao wa matumizi ya barabara kwa lengo la
kuendelea kudhibiti ajali za barabarani pamoja na elimu ya Polisi jamii.
Akiongea
kwa niaba ya Airtel, Meneja Uhusiano wa Airtel Bw, Jackson Mmbando
alisema “ Airtel tumeona ni vyema kuendeleza ushirika wetu na Jeshi la
Polisi usalama Barabarani wakati wote wa mwaka ili
kuhakikisha usalama barabarani unazingatiwa”.Udhamini wetu katika
mashindano haya ya waendesha Bodaboda una lengo la kulinda afya za Watanzania
wanaotumia usafiri wa boda boda, kupitia ushiriki wetu tutafikisha
ujumbe na elimu kwa watumiaji wa barabara kwa kuwa michezo inaleta
hamasa, inaleta burudani , inafanya mwili kuwa imara hivyo kufikiri
vyema, hivyo basi ni matumaini yetu baada ya wiki nzima ya mashindano
ya mpira wa miguu washiriki hawa pia wataweka kukumbuka ya waliojifunza
muda kwa kipindi cha wiki nzima kwa kutii sheria bila shuruti wanapofanya shughuli zao” aliongeza Bw. Mmbando
Naye Mwakilishi wa Mwakilishi wa Rotary club Dar es Saalam Vinay Choudary
alisema “Tumejipanga kupitia michuano hii kusambaza ujumbe juu ya
athari kubwa inayoweka hatarini maisha ya waendesha pikipiki. Tunaamini
elimu ya kutosha ikitolewa kwa vijana wetu wanaofanya biashara za
usafiri kwa njia ya pikipiki kutawaepusha na athari hizi si tu kwa
madereva bali kwa abiria na watumiaji wa usafiri huu kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP. Mohamed Mpinga akizungumziazoezi hili aliwashukuru wadau hao kwa kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua kwa asilimia tano (10%) mwaka huu.
“Tunaendelea
na mikakati mbalimbali tuliojiwekea katika kuhakikisha tunapunguza
ajali za barabarani nchini. Mashindano haya ya waendesha Boda boda ni
moja ya njia tunayoitumia ya kuwafikia walengwa na kutoa elimu kwa
waendesha pikipiki” alisema Kamanda Mpinga.
“Hii
ni nafasi ya kipekee kwetu kuwaweka watumiaji wa barabara karibu ili
tuweze kufikia malengo yetu” alisisitiza kamanda Mpinga .Takwimu
zinaonyesha kuwa mwaka 2012 kulitokea ajali za pikpiki 5763, vifo 930 na majeruhi 5532. Hili ni ongezeko la ajali kwa 7.0%, upungufu wa vifo kwa 1.6% na ongezeko la majeruhi kwa 0.5% ikilinganishwa na mwaka 2011 ambapo kulitokea ajali za pikipiki 5384 zilizosababisha vifo 945 na majeruhi 5506. Kiwango
hiki nikikubwa na kimeleta maafa na hasara kubwa kwa jamii na taifa
kwa ujumla. Tunawashukuru sana Airtel , Rotary club, Baraza la Taifa la
Usalama Barabarani, Mr.Price, Home Shopping Center wadau kwa
kuendelea kushirikiana nasi kuhakikisha tunapunguza kabisa tatizo
hili.Pia tunawashukuru wachezaji kwa timu zao waliojitokeza kupata elimu
na kushiriki mashindano haya kuanzia awamu ya kwanza hadi sasa.
Mashindano haya yanatarajiwa kutimua mbio kuanzia tarehe 28/02/2013
katika viwanja vya Polisi Oysterbey kwa kushirikisha timu 8 zote
kutoka wilaya ya kinondoni ambapo ni muunganiko wa wacheza soka ambao ni
waendesha pikipiki toka vituoni (vijiwe ) vya kinondoni. Mpinga Cup
itaendelea katika mikoa ya Kipolisi ya Ilala na Temeke na hatimaye
kutafuta mshindi wa mkoa wa Dsm.
Kampeni
hizi za Usalama barabarini zitaendelea mfululizo hadi mwisho wa kilele
cha maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa usalama barabarani hapo mwezi
September/Octoba 2013.
No comments:
Post a Comment