UTATA NDANI YA STUDIO YA MHESHIWA JAKAYA.
WIKI iliyopita katika Jukwaa la Wasanii linaloendeshwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), kuliwaka moto kuhusiana na studio aliyoahidi Rais Jakaya Kikwete kwa wasanii hapa nchini.
Mwaka jana wakati akizindua Bunge la 10 mjini Dodoma, Rais Kikwete alisema kuwa amesikia kilio cha wasanii nchini juu ya studio ya kurekodia kazi zao (Mastering Studio) hivyo ameshalitatua hilo kwa kuwapa studio hiyo.
Kauli hiyo ilipokewa kwa furaha na wasanii nchini, wakijua sasa tatizo hilo hawatakuwa nalo tena.
Lakini kadri siku zilivyozidi kwenda, jambo hilo lilianza kuzua maswali yaliyokosa majibu juu ya mahali ilipo studio hiyo na ipo mikononi mwa nani.
Yapo mengi yalizungumzwa juu ya studio hiyo, ikiwa ni pamoja na kutajwa sehemu ilipo na mtu kama si watu wanaoimiliki.
Hapo ndipo suala hilo lilipoanza kuchukua hatua nyingine kwa wasanii kutaka kujua juu ya nani aliyekabidhiwa studio hiyo na kwa nini haijawekwa wazi ni nani anayeimiliki na sehemu ilipo.
Ni kutokana na maswali hayo, Serikali kupitia kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utamaduni wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Angela Ngowi, wiki iliyopita katika Jukwaa la Wasanii, pale Basata, alivunja ukimya.
Ngowi alisema kuwa studio hiyo ilitolewa kwa wale walioomba na si vinginevyo.
“Rais ametoa tamko hilo kwa maandishi, hivyo ni wajibu wa kila msanii kulielewa tamko hilo,” alisema Ngowi.
Ngowi alinukuu kauli hiyo ya Rais Kikwete kama ifuatavyo: “Nimetoa vifaa vya mastering studio kwa ajili ya wasanii walioomba kwangu kupitia risala yao, hata hivyo wasanii wote wanaruhusiwa kuitumia na ikiwa kuna yeyote anahitaji anapaswa kuleta maombi yake.”
Kauli hiyo iliwachanganya wadau waliokuwapo katika
Jukwaa hilo la Wasanii pale BASATA, akiwamo msanii mkongwe nchini ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kupitia tiketi ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA), Joseph Mbilinyi, maarufu kwa jina la Mr II.
Mr II alisema kuwa kama kweli kauli hiyo imetolewa na Rais Kikwete, basi atakuwa hajawatendea haki wasanii nchini na Watanzania kwa ujumla.
“Katika hotuba yake wakati anazindua Bunge la 10 Mjini Dodoma, mwaka jana, Rais Kikwete alisema kuwa amesikia kilio cha wasanii na kuamua kuwapa studio hiyo, lakini tamko lake la hivi karibuni, limepingana na tamko lake la awali,” anasema. “Sasa tunaambiwa eti amewapa wale walioomba, wakati awali alisema amekisikia kilio cha wasanii, akiwa na maana ni wasanii wote wa Tanzania…hapa si bure kuna jambo,” anasema kwa habari bofya hapa....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment