MATOKEO KIDATO CHA SITA YATOKA.
Wavulana wamejitutumua na kufanikiwa kushika nafasi kumi bora katika matokeo ya mtihani wa kidato cha
sita uliofanyika Februari mwaka huu.
Akitangaz amatokeo ya kidato hicho leo, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa, Dk. Joyce Ndalichako alisema, watahaniwa wamejitahidi kufanya vizuri zaidi katika masomo ya hesabati, kemia, jiografia, fizikia, uchumi na biashara kuliko mitihani iliyopita ambapo wengi walikuwa wakaianguka.
Dk. Ndalichako alisema katika mtihani huo, wavulana 25,872 sawa na asilimia 91.690 na wasichana 15,088
sawa na asilimia 92.63 wamefaulu na kutaja wanafunzi kumi bora walioongoza katika matokeo hayo na majina ya shule zao kwenye mabano kuwa ni Muhagachi Chacha (Kibaha), Samwel Katwale (Mzumbe), Amiri Abdalah (Feza Boys), Aron Gerson, Shaban Omary wote wa Tabora Boys, Kudra Baruti (Feza Boys), George Assenga (Majengo), Comman Nduru (Feza Boys), Francis Josephat (Tabora Boys) na George Felix (Mzumbe).
Dk. Ndalichako pia aliwataja wasichana walioongoza kuwa ni Doreen Kabuche (Benjamin Mkapa), Rahabu
Mwang'amba (Kilakala), Mary Moshi (Kifungilo Girls) Nuru Kipato (Marian Girls) Zainabu Hassan (Al-Muntazir Islamic),Catherine Temu (Ashira), Anthonia Lugomo (Usongwe), Cecilia Mville (Kifungilo Girls), Mariam Matolwa (Kilakala) na Suzan Makoi (Tarakea).
Katika hatua nyingine, Dk. Ndalichako alisema shule za sekondari za seminari zimendelea kufanya vizuri
ambapo kwa mara nyingine shule Marian Girls ya mkoa wa pwani imeendelea kutesa kwa kuibuka ya kwanza katika kundi la shule zenye watahiniwa zaidi ya 30.
Alizitaja shule nyengine zilizo kwenye 10 bora katika kundi hilo kuwa ni Feza Boys, Kifungilo, Kibaha, St.
Mary's Mazinde, Ilboru Tabora St. Mary Goreti, Mzumbe na Mafinga na kwa upande wa shule zilizofanya vizuri katika kundi la zile zilizokuwa na watahiniwa chini ya wanafunzi 30 ni Uru Seminary, St. James Seminary, Maua Seminary, Same seminary Dungunyi Seminary D.C.T Jubilee St. Joseph-Kilocho Seminary, Mlama na Masama Girls.
Dk. Joyce akifafanua kuhusu watahaniwa wa mtihani huo mwaka huu alisema jumla ya watahiniwa 44,720
sawa na asilimia 99.47 kati ya waolisajiliwa walifanya mtihani huo ambapo wasichana walikuwa 16,327 sawa na asilimia 99.63 na wavulana 28,393 sawa na asilimia 99.38, huku kuhusu ubora wa ufaulu akisema jumla ya watahiniwa 34,949 sawa na asilimia 78.53 wamefaulu katika madaraja ya kwanza, pili na tatu wakiwemo wasichana 12,868 sawa na asilimia 79 na wavulana 22,081 sawa na asilimia 78.25.
Alisema watahaniwa 49,653 sawa na asilimia 87.24 ya watahiniwa waliofanya mtihani wa kidato cha sita
mwaka 2011 wamefaulu. Wsichana waliofaulu ni 18,351 sawa na asilimia 88.74 wakati wavulana waliofaulu ni 31,302 sawa na asilimia 86.38. Mwaka jana watahiniwa waliofaulu walikuwa 55,772 sawa asilimia 88.85.
Dk. Ndalichako alisema Baraza hilo limefuta matokeo ya watahiniwa watano wa shule na saba wa
kujitegemea waliobainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo.
Kwa matokeo hayo Peruzi www.matokeo.necta.go.tz na www.necta.go.tz au www.moe.go.tz au www.udsm.edu.ac.tz.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment