Kamishna wa Forodha na Ushuru kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Tiagi Masamaki Kabisi akiwaeleza waandishi wa Habari juu ya
faida za Mfumo mpya wa Uondoshaji Mizigo bandarini(TANCIS) ikiwa unasaidia
katika kufanya makadirio ya kodi sahihi kulingana na taarifa sahihi zilizoletwa
kwa kutumia mfumo huo, pia utasaidia wateja kujua sehemu mizigo yao ilipo na
pia wanapaswa kulipa kiasi gani kulingana na mzigo wa mteja, wakati wa Mkutano
na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Ofisa Mwandamizi wa Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) Bw. Felix Tinkasimile akiwaeleza waandishi wa habari namna mfumo
mpya wa uondoshaji mizingo unavyoongeza uwazi na uwajibikaji utakaosaidia
kuzuia upoteaji wa mizigo bandarini ikiwemo Magari na Makontena , wakati wa
Mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Meneja wa Kituo cha Huduma cha Forodha kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Bw. Kasty Phelician akiwaeleza waandishi wa Habari majukumu ya kituo hicho
ikiwemo kutoa tathnimi ya kodi unayopaswa kulipwa kwa kupitia na kuhakiki
nyaraka zote kutoka kwenye kadhia zinazotumia mfumo wa TANCIS ikiwamo viwango
vya ushuru wa forodha vinavyopaswa kutozwa.
Meneja wa Forodha Bandari ya Dar es Salaam kutoka Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA)Bw.Burton Kaissy akiwaeleza waandishi wa Habari namna
wanavyoshirikiana na Taasisi mbalimbali kurahisisha usafirishaji wa mizigo yote
inayoenda nje nchi
No comments:
Post a Comment