Kwa jina halisi alopewa na wazazi wake ni MOHAMMED MUHIYA ila jina analotumia katika sanaa ni SHAUQY MUHIYA ni mwanamuziki wa Qasida Tanzania
Ni
kati ya wasanii wa Qasida wanaofanya vizuri katika Sokoni Kwenye aina
hii ya muziki wa Qasida hapa bongo ambae pia anatamba na video yake ya
AMANI TANZANIA aliyomshirikisha msanii mwenzake mkubwa hapa bongo , iliyofanyika chini ya mikono ya director Mike Tee.
Mbali na kutamba na kibao chake hicho SHAUQY MUHIYA
alieleza kuwa bado anapata changamoto za hapa na pale kama vile,
matatizo za kifedha na Uchache wa upataji matamasha ndani na nje ya
nchi.
Pia alieleza jinsi namna ambavyo mziki umemuonyensha mafanikio kwa hapa alipofikia.
"mafanikio
sio makubwa saaanaa ila naweza nikasema kwa kiasi flani Qasida
imeniongezea mafans na marafiki kibao Duniani. Kingine kikubwa zaidi
naweza nikasema napenda sana mziki hasa wa kumuimbia Mungu,Mbali na muziki ni mwalimu pia wa Quran Tukufu,Matarajio
yangu baadae ni Kuhakikisha jamii nzima inamjua Mungu Na kufata yale
aliyoyaagiza pia kujipatia kipato cha kuendeshea maisha yangu kwa
ujumla.Asante Mngu" Alisema Shauqy Muhiya.
Harakati za muziki za Shauqy zimeanza mwaka 2008 aliporekodi nyimbo yake ya kwanza.
Shauqy kama ilivyo kawaida kwa binadamu kuwapenda wenzetu, yeye mesema kuwa anawakubali saana wasanii wewa Qasida
Tanzania na ameomba wajitokeze wanaopenda kufanya mziki kama huu.
Hivyo wana TANZANIA mnatakiwa kujisifia wasanii/vitu vya kwenu na kuvipenda kwa kuvijenga zaidi kupitia kukosoa kwenu, na kuzipromoti kazi zao
Msikilize hapa ikiwezekana umpatie sapoti ili aweze kurekodi album hii kali yenye baraka tele.
SIKILIZA NA DOWNLOAD Bonyeza HAPA
Msikilize hapa ikiwezekana umpatie sapoti ili aweze kurekodi album hii kali yenye baraka tele.
SIKILIZA NA DOWNLOAD Bonyeza HAPA
No comments:
Post a Comment