Mtaalam
wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi kutoka kituo cha mazingira cha
Finland akitoa maelezo kwa baadhi ya viongozi wa Tanzania kuhusu htu
zinazochukuliwa na nchi hiyo katika kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi.
Viongozi
wa Tanzania wakiwemo mameya na wakurugenzi wa majiji sita ya Tanzania
walioko nchini Finland kwa ziara ya mafunzo inayoratibiwa na taasisi ya
Uongozi ya Tanzania wakipata maelezo kuhusu aina mpya ya gari
inayoendeshwa kwa kutumia umeme iliyoko katika kituo cha mazingira cha
Finland kiitwacho Helsinki Environmental centre.
Na Vedasto Msungu wa ITV Finland
Viongozi wa wa Tanzania wakiwemo mameya na wakurugenzi wa
majiji sita ya Tanzania walioko katika ziara ya mafunzo nchini Finland wametembelea
kituo cha mazingira cha nchi hiyo kiitwacho Helsinki Environmetal centre
kujifunza kuhusu hatua zinazochukuliwa na nchi hiyo kukabiliana na tatizo la
mabadiliko ya tabianchi.
Wakongea na viongozi hao kutoka majiji sita ya Tanzania
ikiwemo Dar Es salaam, Mbeya, Mwanza, Arusha, Tanga na Zanzibar, watendaji wa
kituo hicho wamesema nchi hiyo imeanza kuchukua hatua mbalimbali ili
kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabianchi.
Wamezitaja hatua hizo kuwa ni pamoja na kutilia mkazo
suala la upandaji miti lakini pia kumeanzishwa mpango wa matumizi ya magari
yasiyohitaji kutumia mafuyt ya dizeli au petrol ambayo sasa yanaendeshwa kwa
kutumia umeme.
Kwa mujibu wa wataalam wa mazingira wa kituo hicho, hatua
hizo zinalenga kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa unaotokana na ongezeko la
shughuli za binadamu ikiwemo moshi wa viwanda, magari na ukataji miti ovyo.Wamesema matumizi ya magari hayo yanayoendeshwa kwa
kutumia umeme yanaendelea kuongezeka na kwamba katika nchi hiyo kuna vituo
zaidi ya 50 vya kuchaji magari hayo kwa umeme na pia kila raia wa Finland
anaemiliki gari ya aina hiyo anaweza kuchaji gari nyumbani kwake.
Aidha wametaja matumizi ya vioo vya madirisha au milango
ambayo imewekwa vioo maalum vinavyofungwa kwenye madirisha au milango lakini
wakati huo huo ni panel za sola zinazozalisha umeme na kutumika kw shughuli
mbalimbali ikiwemo viwandani na majumbani.
Wametaja mfano katika jingo lao kuwa panel za sola
zilizoko kwenye milango na madirisha zinazalisha umeme mwingi ambao hutumika
kwa shughuli za ofisi na unaobaki unaingizwa katika gridi ya taifa kwaajili ya
watumiaji wengine.
No comments:
Post a Comment