Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu
(katikati) akiingia katika kongamano la majadiliano kuhusu changamoto za
kufikika kwa huduma za fedha kwa wajasiriamali wadogo na wa kati
Tanzania jijini Dar es Salaam Jumanne wiki hii. Wengine ni Katibu
Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), Bw. Raymond Mbilinyi
(kushoto) na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey
Simbeye (Kulia). Kongamano hilo lilitayarishwa na TPSF pamoja na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha Tanzania (FSDT).
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye (Kushoto) akitoa hotuba yake wakati wa kongamano
la majadiliano kuhusu changamoto za kufikika kwa huduma za fedha kwa
wajasiriamali wadogo na wa kati Tanzania jijini Dar es Salaam Jumanne
wiki hii. Kulia ni Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu;
Katibu Mtendaji wa Baraza la Biashara la Taifa (TNBC), Bw. Raymond
Mbilinyi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa VICOBA na Mbunge Viti
Maalum, Bi.
======== ======== ==========
Taasisi
za fedha nchini zimeshauriwa kulegeza masharti ya utoaji mikopo ili
wajasiriamali nchini waweze kupata fursa zaidi ya kupata mitaji
kuendeleza biashara zao na kushiriki katika ujenzi wa uchumi wa nchi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dkt. Mary Nagu
alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kufungua Kongamano la majadiliano kuhusu changamoto za kufikika kwa
huduma za fedha kwa wajasiriamali wadogo na wa kati Tanzania jijini Dar
es Salaam. Waziri huyo alisema Jumanne wiki hii kuwa taasisi za
fedha nchini zilegeze masharti ili wajasiliamali waweze kupata mitaji ya
biashara zao.
Kongamano
hilo lilitayarishwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa
kushirikiana na Financial Sector Deepening Trust (FSDT). “Ninayo
furaha kubwa kuona TPSF na wadau wengine wameandaa kongamano hili ambalo
linalenga kutafuta suluhisho la wajasiliamali kupata mitaji kutoka
taasisi za fedha,”alisema.
Alisema
moja ya changamoto ambazo wajasiriamali wanakumbana nazo ni namna ya
kupata mitaji kutoka katika taasisi hizo, jambo ambalo linarudisha nyuma
maendeleo ya biashara. Alisema mikopo kutoka benki inatolekewa kwa masharti makubwa na riba kubwa jambo ambalo ni kikwzo kwao na taifa pia.
“Sera
ya nchi inaruhusu sekta binafsi kuendesha uchumi kupitia kampuni ndogo,
za kati, na wajasilimali, sasa mitaji kwa wajasiriamali ni jambo ambalo
haliepukiki,”alisema. Alisema serikali inashirikiana na TPSF
kuhakikisha mazingira ya biashara yanaimarika na kongamano hilo ni moja
ya hatua muhimu katika kuondoa vikwazo hivi.
Aidha
alisema wakati nchi inasubiri kuingia katika uchumi mkubwa kutokana na
gesi na mafuta ni lazima wajasiriamali wadogo wawezeshwe ili pia wawe na
uwezo wa kutoa huduma kwa kampuni kubwa. Kwa upande wake,
Mkurugenzi Mtendaji TPSF, Bw. Godfrey Simbeye alisema kongamano hilo ni
la muhimu katika kutafuta ufumbuzi wa mitaji kwa wajasiliamali ambao ni
tegemeo kubwa katika kuendeleza nchi.
“Nchi zilizofanikiwa zimewekeza katika maendeleo ya wajasiriamali wao, hatuna budi kufanya hivyo,” alisema. Alifafanua kuwa wajasiriamali wakipatiwa huduma za fedha na kukuza mitaji yao, wana nafasi kubwa ya kuleta maendeleo.“Tumeshuhudia ukuaji wa mitaji na uchumi wetu unakwamishwa na mambo mengi mojawapo ni namna ya kupata mitaji,”alisema.
Alisema
mitaji mingi inatoka benki lakini kwa mazingira yaliyopo ni vigumu kwa
biashara inayoanza kupata mitaji kutokana na masharti ambayo siyo
rafiki. Alisema sekta hiyo lazima iwezeshwe sababu ndiyo yenye uwezo wa kutoa jira kubwa na kuleta mapinduzi ya uchumi.
Naye
Mtaalamu wa Maswala ya Wajasilimali, kutoka FSDT, Bw. Peter Kingu
alisema kuna kila sababu taasisi za fedha kupanua wigo kwa wajasilimali
kupata mitaji bila ya kuweka masharti magumu. “Taasisi yetu
inafanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo TPSF katika
kuhakikisha wajasiriamali wanaimarika kibiashara,” alisema.
Kongamano
hilo lilishirikisha wadau mbalimbali toka sekta binafsi, sekta ya umma,
taasisi za utafiti, kampuni mbalimbali pamoja na benki miongoni mwa
wadau wengine. Kampuni ya simu za mkononi ndiyo iliyodhamini
kongamano hilo. Inatarajiwa kuwa maazimio ya kongamano hilo yatasaidia
katika juhudi za kurahisisha upatikanaji wa huduma za fedha miongoni mwa
wajasiriamali wadogo na wa kati hapa nchini
No comments:
Post a Comment