Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib
Bilal akiagana na Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika, baada
ya shughuli za maadhimisho ya Sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Malawi
kukamilika katika uwanja wa Civo, jana Julai 06, 2014. Nyuma yake ni
Mama Asha Bilal. Picha na OMR.
Wa pili (kushoto) ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Rais wa Malawi Profesa
Arthur Mutharika akifuatiwa na mkewe, Mheshimiwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha
Bilal na viongozi wengine wakifuatilia sala maalum ya kuombea nchi ya
Malawi wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo zilizofanyika
jana Jumapili Julai 06, 2014 katika uwanja wa Civo jijini Lilongwe,
Malawi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib
Bilal akiongozana na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Klaus
Chilima kukagua gwaride maalum la makaribisho kwa Mheshimiwa Makamu wa
Rais wa Tanzania baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Lilongwe
kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi
zilizofanyika Jumapili tarehe Julai 06, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyeji wake
Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Klaus Chilima, wakifurahia ngoma za asili za
Malawi, wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa Lilongwe, alipowasili
kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi zilizofanyika Jumapili
tarehe Julai 06, 2014.
No comments:
Post a Comment