Waziri wa
Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akipongezana na Balozi Chales
Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB
mara baada ya kuzindua rasmi SITE ya Maonyesho ya Kimataifa Utalii ya
Tanzania yanayojulikana kama Swahili International Tourism Expo (SITE)
kwenye hoeli ya Serena Mwisho ni mwa wiki, Maonyesho
hayo yatakayohusisha kampuni binafsi, taasisi za kiserikali kama Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB) pamoja na washirika wengine katika sekta hiyo
yanatarajiwa kufanyika tarehe 1 mpaka 4 Oktoba, mwaka huu katika ukumbi
wa Mlimani City Dar es Salaam, Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya
Utalii Bi. Devotha Mdachi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-DAR ES
SALAAM)
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akizungumza katika zinduzi huo wakati alipokuwa akisoma hotuba yake.
Wageni wlikwa mbalimbali wakiangalia jinsi mabanda yatakayotumiwa na washiriki wa maonyesho yatakavyokuwa.
Balozi Chales Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB akimkaribisha Waziri Razalo Nyalandu ili azungumze na kisha kuzindua maoyesho hayo.
Seraphin Lusala Mkurugezni wa Masoko na Mauzo Serena Hotel kulia akiwa katika hafla hiyo. Balozi Chales Sanga Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB kulia akiwa pamoja na wageni wengine katika hafla hiyo. Wageniwaalikwa mbalimbali wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla hiyo. Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akiwa pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii TTB Bi. Devotha Mdachi na kulia ni Beatrice Mwiru Ofisa Masoko wa bodi hiyo.
Meneja wa
Masoko Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena Katikati, Emmanuel
Okware Meneja wa mauzo kutoka Quatar Airways kulia na mdau Juma Mabakila
wakiwa katika hafla hiyo. Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akizungumza na Bi. Lima D'Silva Mwakilishi wa mauzo Ethiopian Airlines.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Razalo Nyalandu akisalimiana na wageni mbalimbali waliohudhuria katika haf hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano Bw. Goefrey
Tengenea wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na maofiza
wenzake wa TTB wakati wa hafla hiyo.
................................................................................................
(HOTUBA YA MH. WAZIRI RAZALO NYALANDU WAKATI WA UZINDUZI WA SITE)
Napenda kuchukua nafasi hii kutoa
shukrani zangu za dhati, kwa wageni wote mliofika katika tukio hili
muhimu ambapo nitatambulisha kwenu kuanzishwa kwa onesho jipya la utalii
la kimataifa litakalojulikana kwa jina la Swahili International Tourism
Expo (S!TE).
1. Sekta ya Utalii ni kichocheo kikubwa
cha ukuaji wa uchumi hasa kwa kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za
kiuchumi kama vile usafirishaji, viwanda na biashara, kilimo, sanaa za
mikono na kadhalika. Sekta ya utalii ina uwezo wa kuongeza ajira kwa
haraka zaidi na inatambulika kwamba kila mtalii mmoja anapokuwa nchini
huchangia takribani nafasi 12 za ajira za aina mbalimbali. Aidha, Utalii
ni tasnia muhimu katika kuongeza kipato na kupunguza umasikini, kukuza
mahusiano ya kijamii na vile vile katika kutunza na kuendeleza maeneo ya
kihistoria na maliasili. Hapa nchini, katika kipindi cha kati ya mwaka
2002 na 2013, utalii wa kimataifa umekuwa kwa zaidi ya asilimia 50%,
kutoka watalii 575,000 mwaka 2002 wambao waliliingizia taifa Dola za
Marekani milioni 730 hadi kufikia watalii 1,135,884 mwaka 2013 ambao
waliingizia taifa Dola za marekani Bilioni 1.81.
2. Tanzania imebarikiwa kwa kuwa na
vivutio vya maliasili na utamaduni vya kipekee. Kutokana na kuwepo kwa
vivutio hivi, taasisi ya Kimataifa ya World Economic Forum katika
taarifa yake ya ushindani kwenye tasnia ya Utalii (Travel and Tourism)
imeitaja Tanzania kuwa ni nchi ya pili (2) duniani ikiongozwa na Brazili
kwa kuwa na mazingira asilia yenye Urithi asilia wa kimataifa, wingi wa
wanyamapori na ardhi kubwa iliyo hifadhiwa. Hakika, ni ukweli
usiopingika kwamba katika vivutio saba vya maajabu ya asili katika bara
la Afrika, vitatu vinatoka Tanzania. Huu ni ushuhuda kwamba juhudi zetu
za kuhifadhi mazingira zinazaa matunda. Hivi sasa Bonde la Ngorongoro;
hifadhi ya Taifa ya Serengeti, na Mlima Kilimanjaro ni vivutio ambavyo
vimeorodheshwa katika Maajabu saba ya asilia barani Africa.
3. Hata hivyo, hatuwezi kutegemea tu
uwingi na ubora wa vivutio hivi vya utalii peke yake. Ni muhimu kuongeza
juhudi zaidi kuliko wakati mwingine wowote, ili kujenga uelewa wa
utajiri huu kidunia. Kama taifa, tunahitaji juhudi na mikakati zaidi ili
kutangaza vivutio vyetu.
4. Kwa kuzingatia umuhimu wa kuendelea
kutangaza utalii wetu na kuifaya Tanzania iweze kushindana kimataifa,
mnamo mwezi Februari, 2013, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), iliingia
makubaliano na kampuni inayojulikana kama Pure Grit Project and
Exhibition Management LTD, hapo mwanzo ilijukana kama Witch & Wizard
Creative (Pty Ltd) ili kuanzisha maonyesho ya utalii ya kimataifa
nchini Tanzania yajulikanayo kama Swahili International Tourism Expo
-S!TE), ambayo yataanza rasmi Mwezi Oktoba, 2014. Pure Grit Project and
Exhibition Management LTD ni kampuni inayoendesha maonesho ya utalii ya
INDABA ambayo ni maonesho ya tatu kwa ukubwa duniani. Onesho la S!TE
litafanyika hapa Dar es salaam, mwezi Oktoba kila mwaka katika ukumbi wa
mikutano wa Mlimani City na kujikita zaidi katika kuvutia washiriki
kutoka ndani nan je ya nchi.
5. Mkoa wa Dar es Salaam umechaguliwa
mahsusi kuwa eneo la kufanyika kwa onesho la S!TE kutokana na sehemu
ulipo Mkoa huo kijiografia, na uwepo wa miundombinu bora na huduma nzuri
zinazofaa kwa kuendesha au kuanzisha maonyesho ya utalii ya kimataifa.
6. Hadi kufikia Juni 2014, hali ya maandalizi ya onesho hili ni kama ifuatavyo.
6.1 Mwenendo wa idadi ya washiriki hadi
sasa: Zaidi ya asilimia 50% ya nafasi za maonesho hayo tayari zimejazwa
kwa kuchuliwa na makampuni binafsi na Bodi za Utalii za nchi mbalimbali.
Aidha, kuna idadi kubwa na ya kuridhisha ya maombi ya washiriki
inayoendelea kuandaliwa. Lengo ni kwamba ifikapo katikati ya mwezi
Agosti, 2014 tuwe tumetumefikia asilimia 100.
6.2 Programu maalum ya kuwaleta nchini
wakati wa maonesho hayo mawakala wakubwa wa biashara ya Utalii: Katika
kuhakikisha kuwa onesho hili linakuwa ni fursa ya kuwaunganisha
wafanyibiashara ya Utalii wa Tanzania na masoko ya Utalii, S!TE itakuwa
na programu maalum (Hosted buyer and travel writer programme) ya
kuwaleta nchini wakati wa maonesho hayo mawakala wakubwa wa biashara ya
Utalii na waandishi wa habari za utalii (Tour Operators, Wholesalers,
Packagers and Travel Agents and Travel Writers) na kuwapangia ratiba
maalum ya kuonana na washiriki wa maonesho hayo ili kuwawezesha
kuanzisha uhusiano wa kibiashara. Mawakala hao wapatao ishirini na
wandishi wa habari kumi watagharimiwa (hosted) na S!TE.Hadi kufikia Juni
2014,mawakala 13 kutoka Marekani, Australia, Ujerumani, Uholanzi,
India, Mexico, Norway na China wamethibitisha ushiriki wao.
6.3 Utangazaji wa Onesho la S!TE: Onesho
la S!TE lina tovuti ijulikanayo kama www.site.co.tz. Tovuti hii
imeandaliwa ili kukidhi maudhui ya onesho lenyewe ambapo inataarifa
nyingi zinazoweza kumfanya yeyote anayetembelea tovuti hiyo kupata
taarifa zote muhimu kwa muda mfupi. Kwa mfano tovuti inatoa taarifa za
ukumbi wa onesho, mabanda ya maonesho yatayojengwa na kumruhusu mteja
kuchagua eneo kulingana na uwezo wake. Aidha, tovuti hii ambayo pia
imeunganishwa na ukurasa wake wa Facebook, inapatikana kwa lugha
mbalimbali
7. Pamoja na kuitangaza Tanzania kama
kituo muhimu cha utalii katika ukanda wa Afrika ya Mashariki, S!TE ina
lengo la kuunganisha wafanya biashara wa Utalii wadogo na wa kati wa
Tanzania (Small and Medium Tourism Enterprises - SME’s), na masoko ya
utalii ya kimataifa. Ni ukweli kwamba SME’s za kitanzania zina uwezo
mdogo wa kimtaji wa kuweza kufikia masoko ya utalii ya kimataifa.
Kupitia S!TE, hasa kupitia programu maalum ya kuwaleta nchini wakati wa
maonesho hayo mawakala wakubwa wa biashara ya Utalii, itasaidia katika
kutatua changamoto hii.
Naomba watanzania kuchangamkia fursa hii muhimu katika kukuza biashra ya Utalii nchini.
No comments:
Post a Comment