Meneja
wa kituo cha Sengerema FM Redio, Ndg. Felician Ncheye, akitoa nasaha za
ukaribisho kwa washiriki wa mradi wa SHUGA na mgeni rasmi. Katikati ni
Mgeni rasmi Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza
kupitia mradi wa TACAIDS, Ndg. Geofrey Mabu na Kulia ni Afisa Mipango
VVU/UKIMWI UNESCO, Ndg. Herman Mathias.(Picha zote na Zainul Mzige wa
MOblog).
Na Mwandishi wetu, SENGEREMA - MWANZA
Redio
za jamii nchini zimeaswa kutumika vizuri katika kuelimisha kamii juu ya
kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kupitia vipindi vya
redio. Hamasa hiyo imetolewa na Ndg Geofrey Mabu
ambaye ni mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza
kupitia mradi wa TACAIDS wakati akifungua warsha ya siku tatu ya mradi
mpya ujulikanao kama SHUGA, unaotekelezwa na shirika la Elimu, Sayansi
na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana Shirika la Mfuko wa Watoto
(UNICEF) inayofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema mkoani
Mwanza.
Mabu
amesema kuwa mradi huo umekuja wakati muafaka ambapo malengo yake
yakizingatiwa na kutekelezwa kama ilivyopangwa utasaidia kufikia malengo
ya serikali ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI hadi Zero.
Mgeni
rasmi Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia
mradi wa TACAIDS, Ndg. Geofrey Mabu akifungua warsha ya siku tatu ya
mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU
ujulikanao kama SHUGA.
Amesema
kuwa redio za jamii ni kiungo muhimu katika kuelimisha jamii na kuwa
kama zitatumika vizuri kusambaza elimu ya UKIMWI kupitia vipindi vyake
zitasaidia kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali kupitia TACAIDS.
Vile
vile ameziomba redio zitakazoshiriki katika mradi huu, kutumia vizuri
fursa hii waliyoipata kuhakikisha wanafanikisha malengo ya mradi kwa
kiwango cha juu kwa kufanya hivyo pia watakuwa wamelinusuru taifa na
janga hili la UKIMWI.
Mshauri
na Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Bi. Rose Haji Mwalimu akitoa
maelezo kuhusu madhumuni ya warsha inayohusisha mradi wa SHUGA.
Awali
Mkufunzi wa Radio za jamii kutoka shirika la UNESCO Bi Rose Mwalimu
akitoa ufafanuzi wa malengo ya semina hiyo, amesema kuwa mradi huu wa
SHUGA unalenga kupambana na maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI kwa
vijana hapa nchini kupitia vipindi vya mchezo wa redio kubadili tabia.
Amezitaja
redio 10 zinazoshiriki katika mradi huu nchini Tanzania kuwa ni FADECO
Redio ya Karagwe mkoani Kagera, ORS ya Manyara, Sengerema FM mkoani
Mwanza, Pangani FM ya mkoani Tanga na Kahama FM kutoka Shinyanga. Nyingine
ni Kitulo FM ya Makete Njombe, Kyela FM ya Mbeya, Nuru FM kutoka
Iringa, Pambazuko FM Ifakara na Kwanza Jamii Redio FM kutoka Njombe.
Afisa
Mipango VVU/UKIMWI UNESCO, Ndg. Herman Mathias akitoa mada kuhusu
VIjana, Balehe na Mahusiano ya Ngono wakati warsha ya siku tatu ya mradi
mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU
ujulikanao kama SHUGA.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia kwa umakini mada zilizokuwa zikitolewa na wakufunzi.
Mshiriki kutoka Kahama FM Redio, Makunga Peter akiuliza jambo kutoka kwa mkufunzi (hayuko pichani).
Afisa
Mipango VVU/UKIMWI kutoka UNICEF, Bi. Alice Ijumbe akitoa mada kuhusu
kiwango cha Maambukizi ya VVU kwa Vijana na hali ya Afya ya Uzazi Salama
wakati wa mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment