Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimuomba Balozi Mteule wa
Tanzania Nchini Sweeden Balozi Dora kuitanga sera ya Utalii Zanzibar
kwenye taasisi na mashirika ya kigeni awapo kwenye utumishi wake Nchini
Sweeden.Mazungmzo hayo yalifanyika ofisini kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.
Balozi
Mteule wa Tanzania Nchini Sweeden Balozi Dora Msechu wa pili kutoka
kushoto aliyevaa nguo rangi ya njano akiaga rasmi kwa Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baada ya kuchanguliwa kushika wadhifa huo wa Kidiplomasia.Picha na Hassan Issa-Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
---
Ofisi
za Kibalozi za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zimekumbushwa kuendelea
kuitangaza Sera ya Utalii iliyoanzishwa na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar katika mpango wake wa kuimarisha uchumi ili kuacha tegemezi la
zao moja la karafuu ambalo baadhi ya wakati hupata changamoto
inayosababisha kutetereka kwa mapato ya Taifa.
Kumbusho
hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati wa mazungumzo yake na
Balozi Mteule wa Tanzania Nchini Sweeden Mh. Dora Msechu aliyefika
kumuaga akijiandaa kwenda kutekeleza kazi yake mpya aliyokabidhiwa na
Taifa.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alimtaka Balozi Dora kuitangaza
vyema Zanzibar Kiutalii wakati zinapotokea fursa za uwekezaji kwenye
mataifa anayokwenda kufanya kazi akiiwakilisha Tanzania.
Alieleza
kwamba Zanzibar hivi sasa inategemea zaidi Diplomasia ya kiuchumi
katika kuimarisha mipango yake ya maendeleo ya Taifa na ustawi wa jamii
kwa kushirikiana na Mashirika, Taasisi na Mataifa mbali mbali rafiki
na hisani.
“
Wewe ndie sikio letu, Wewe ndie mwakilishi wetu kwenye eneo la
kidiplomasia katika kutetea maslahi ya Taifa “. Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar alimtanabahisha Balozi Dora.
Balozi
Seif alielezea faraja yake kutokana na uteuzi aliyopata Balozi Dora
Msechu ambae si mgeni katika shughuli mbali mbali za Kidiplomasia
alizozianza mwanzoni mwa ajira yake.
Alimuomba
Balozi huyo Mteule wa Tanzania Nchini Sweeden kuwasiliana na taasisi
zinazosimamia sekta ya utalii ili kupata vielelezo vya kina
vinavyofafanua hali halisi ya mazingira na vivutio vya uwekezaji katika
sekta ya Utalii hapa Zanzibar.
Mapema
Balozi Mteule wa Tanzania Nchini Sweeden Mh. Dora Msechu alisema
heshima aliyopewa na Taifa imempa faraja kubwa iliyotowa fursa kwake
kujiandaa kufanya kazi kwa nguvu zake zote.
Balozi
Dora alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
kwamba muda wote yuko tayari kupokea agizo, mawazo na busara za
waliomtangulia katika utumishi wa umma ili atekeleze kazi zake kwa
kujiamini.
Akigusia
sekta ya Utalii iliyopewa nafasi kubwa ya kuchangia uchumi wa Zanzibar
Balozi Dora Msechu aliitanabahisha Serikali pamoja na viongozi
wanaosimamia sekta hiyo kuhakikisha kwamba suala la amani na usalama wa
wawekezaji ndio jambo la msingi katika utekelezaji wa sera hiyo.
Balozi
Dora alisema ukosefu wa mambo hayo mawili muhimu ni kusema kwamba kasi
na nguvu za Serikali katika kuimarisha sekta hiyo inaweza ikawa ya bure
na kupoteza nguvu na fedha nyingi bure.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
22/5/2014.
No comments:
Post a Comment