IKIWA
na lengo la kudhibiti wizi wa kazi za Sanaa hapa nchini, Kampuni ya
Msama Promotions ya jijini Dar es Salaam, inatarajia kufungua maduka
katika majiji manne hapa nchini baada ya Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama maduka
hayo yatakuwa katika majiji ya Arusha, Mbeya, Mwanza na mkoani Dodoma
ambayo yatakuwa yakiuza kazi halisi za wasanii.
Msama
alisema kwa kuanzia wataanza na jiji la Mwanza, ambako wanatarajia
kuweka duka katika mitaa ya Nyerere na Libert jijini humo.
Aidha
Msama alisema mashabiki wengi wanauziwa DVD feki nyingi ambazo
wanauziwa kati ya shilingi 1000-1500 ambazo zinadumu wii mbili wakati
kazi halisi wanaziuza kwa bei ya jumla shilingi 2000 na rejareja
shilingi 3000.
Msama
alisema kwa jiji la Dar es Salaam, kampuni yake ina maduka katika
maeneo ya Kariakoo mtaa wa Msimbazi naMasasi lingine lipo Posta Mpya
mtaa wa Mkwepu
No comments:
Post a Comment