Hatimaye
kikosi cha Manchester City kilicho chini ya kocha mkuu ‘Manuel
Pellegrini’ kimeweza kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya England maarufu
kama EPL baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2 – 0 dhidi
ya wagonga nyundo wa jiji la London Westham United katika mtanange wa
mwisho wa kufunga pazia la ligi kuu hiyo inayoongoza kwa kutazamwa na wapenzi wengi wa soka Duniani.
Wachezaji
wa Manchester City wakiwa wamemnyanyua juu kocha wao Manuel Pellegrini
ikiwa ni ishara ya kuonyesha ni jinsi gani walivyokuwa na furaha
Mabao ya City yalifungwa na Samir Nasir baada ya kupewa pasi
nzuri kutoka kwa kiungo mshambuliaji Yaya Toure huku goli la pili
likifungwa na Vicent Kompany. Mchezo mwingine uliokuwa wa vuta nikuvute
ni ule ulioikutanisha klabu ya Liverpool waliowakaribisha nyumbani
NewCastle United ambao walikubali kipigo cha bao 2 -1 kutoka kwa majogoo
hao wa London katika mtanange uliochezwa kwenye dimba la Anifield
jijini humo.
Magoli
ya Liverpool yalifungwa kupitia mshambuliaji wake hatari Daniel
Sturridge pamoja na Daniel Agger aliyesawazisha huku bao pekee la
kufutia machozi kwa Newcastle likipatikana baada ya mchezaji wa
Liverpool Martin Skrtel kujifunga wakati akijaribu kuokoa mpira.
Wachezaji wa Liverpool wakiwa
wamekosa furaha licha ya ushindi wa bao 2 -1 dhidi ya NewCastle lakini
haikuwa muarobani kwa Man City walioibuka mabingwa
Matokeo hayo yameiwezesha Manchester City kutwaa ubingwa huo
mkubwa kwa mara ya pili ndani ya misimu mitatu wa mwaka 2011/12 pamoja
na 2013/14 huku ikimaliza kileleni mwa ligi hiyo kwa jumla ya pointi
86, wakati wapinzani wao wanaowafuatia ‘Liverpool’ wakiwa nyuma yao
kwa tofauti ya pointi mbil tu huku Norwich City, Fulham pamoja na
Cardiff zikijikuta zikishuka daraja.
mashabiki wa Liverpool wakiishangilia timu yao
Michezo mingine iliyochezwa leo ni pamoja na Cardiff
iliyokubali kipigo cha bao 1 -2 toka kwa Chelsea, Fulham ikitoka sare ya
2 – 2 na Crystal Palace wakati Norwich ikiloweshwa goli 0 – 2 kutoka
kwa washika mtutu wa jiji la London ‘Arsenal, Southampton ikiilzamishana
sare ya bao 1 – 1 na Manchester United, Sunderland wakichezea bao 1 – 3
toka kwa Swaswea City, Tottenham Hotspurs ikiigalagaza 3 -1 Aston Villa
na mwisho kabisa ni West bromwich Albion iliyopokea kipigo cha 1 – 2
toka kwa Stoke City.
No comments:
Post a Comment