Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Maunt Meru, mkoani Arusha Mchungaji Profesa Harrison
Olang' (kulia), akishikana mikono na Meneja Mauzo na Usambazaji wa
Kampuni ya Bia Tanzania TBL), Bw. Devis Deogratius, baada ya kampuni
hiyo kutoa miti 1300 kwa ajili ya mkoa wa Arusha, ambapo miti 1250
ilipandwa Chuoni hapo na miti 50 ilipandwa kwenye kiwanda cha TBL.
Meneja
Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), mkoani Arusha Bw.
Devis Deogratius (aliyepiga magoti), akishiriki kupanda moja ya miti
1250 iliyotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya mkoa wa Arusha, baada ya
kampuni hiyo kutoa miti 1300 kwa Manispaa ya Arusha, ambapo miti 1250
ilipandwa Chuoni hapo na miti 50 ilipabswa kwenye kiwanda cha TBL
Arusha.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Maunt Meru, mkoani Arusha Mchungaji Profesa Harrison
Olang' (aliyepiga magoti kushoto), akishiki kupanda miti 1250 chuoni
hapo, iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kwa ajili ya
Manispaa ya Arusha. Wanaoshuhudia katika picha ni baadhi ya wafakazi wa
TBL na wafanyakazi wa Chuo hicho.
Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Bi. Stella Kaaya akishiriki kupanda moja ya
miti 1300 iliyopandwa katika Chuo Kikuu cha Maunt Meru, mkoani Arusha,
iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Kaimu
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Bi. Stella Kaaya (kulia) akimsikiliza kwa
makini Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Maunt Meru mkoani Arusha Mchungaji Profesa
Harrison Olang' (kushoto), baada ya kushiriki zoezi la kupanda miti
1300 kwenye eneo la Chuo hicho, iliyotolewa na Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL).
No comments:
Post a Comment