Nigeria imetajwa kuwa nchi ya kwanza kuongoza kiuchumi barani
Afrika na kuipita Afrika kusini iliyokuwa ikishikilia nafasi ya kwanza
hapo awali.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotangazwa na waziri wa fedha wa
Nigeria, Ngozi okondwe ileyala alisema ‘’Nigeria ni nchi inayodhalisha
mafuta kwa wingi barani Afrika na hivi sasa inachukua nafasi ya 26
katika orodha ya nchi zenye uchumi mkubwa duniani’’.
Wakati huo huo shirika la fedha la kimataifa ‘IMF’ pamoja na
mashirika mengine ya fedha ya kimataifa yameidhinisha takwimu mpya za
GDP ambazo zimeifanya nchi hiyo kuongoza kiuchumi barani afrika.
Pato la taifa ka Nigeria kwa mwaka jana liliongezeka na
kufikia dola za kimarekani bilioni 509.9 ikiwa ni juu ikilinganishwa na
Afrika kusini.
No comments:
Post a Comment