Baadhi
ya Wananchi wa kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa
Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,wakimsikiliza Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana alipozungumza nao kabla ya kukagua mradi
mkubwa wa soko la Samaki (Mwalo),ambao imeelezwa kuwa utapunguza
umaskini kwa kiasi kikubwa kwa baadhi ya wakazi wa eneo hilo. Hata hivyo
imeelezwa kuwa mradi huo wa soko na kuhifadhia samaki umechelewa
kukamilika na kupitisha miaka miwili ya zaidi ya muda ulipangwa kwenye
mkataba,Kinana amewahidi Wananchi kuwa atalifuatilia tatizoo hilo na
kuhakikisha mradi huo unakamilika kama ilivyoahidiwa.Eneo hilo la kisasa kabisa litatumika kuongeza thamani ya samaki.
Mmoja
wa wakazi wa kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa
Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,akiuliza swali la zahanati na
,Elimu na Barabara kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana
(pichani kulia),alipozungumza nao kabla ya kukagua mradi mkubwa wa
Samaki (Mwalo).
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishirikii ujenzi wa mradi wa soko la samaki
(Mwalo),katika kijiji cha Ikola,kilichopo pembezeni mwa Ziwa
Tanganyika,Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi,
Kinana akipata maelezo mafupi kuhisiana na eneo la soko hilo la kukaushia samaki na dagaa
Ndugu Kinana akikaribisha kwa balozi.
Ndugu
Kinana na Ujumbe wake wakiwa wameketi kwa balozi wa shina namba 2,tawi
la Ikolasto katika kijiji cha Ikola,Wilayani Mpanda jioni ya leo mkoani
Katavi.
Ndugu
Kinana akizungumza na wajumbe wa shina namba 2 (hawapo pichani),tawi la
Ikolasto katika kijiji cha Ikola,Wilayani Mpanda jioni ya leo mkoani
Katavi.
Wajumbe wa tawi la Ikolasto wakimsikiliza katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana.(hayupo pichani).
Mbunge
wa Mpanda Vijijini, Moshi Kakoso, akijibu na kutoa taarifa mbalimbali
kuhusiana na jimbo lake katika suala zima la kutekeleza na kuhumiza
Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010,mbele ya wakazi wa kijiji cha
Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo.
Katibu
wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Kapalamsenga,wilayani Mpanda mkoani Katavi jioni ya leo,katika mkutano
wa hadhara,Kinana alijikuta akigeuka mbogo na kuwaomba radhi wakazi wa
kata ya Kirema, Ikola na Kapalamsenga,wilayani Mpanda
mkoani Katavi, baada ya kubaini kuwa,kumekuwepo na kutowajibika kwa
baadhi ya watendaji wa Serikali.Kinana amesema chama
chake kamwe hakitowavumilia watendaji wanaoendekeza vitendo vya urasimu
na
umangimeza wa kutumia makaratasi ofisini badala ya kuwatumikia wananchi
kwa
kuwajibika ipasavyo.
No comments:
Post a Comment