Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwapungia wananchi
alipowasili kwenye maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa chama hicho
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, jijini Mbeya leo. Kushoto kwake
ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. JK aliimpongeza Kinana kwa
kuonesha njia na kutoa mfano kuhusu kufanya kazi ya chama ndani ya
umma. Katika ziara zake mikoani akifduatana na baadhi ya makatibu wa
Sekretarieti na viongozi wengine wa CCM, amekuwa anafanya kazikubwa na
nzuri sana . Na kwamba ziara zake zinakijenga chama na kutoa tawsira
nzuri ya chama katika jamii. Pia alisema ziara za Kinana zinahuisha uhai
wa chama.
Ndugu Kinana amekuwa anafanya mambo ambayo hayajazoeleka kufanywa.
ametembelea maeneoa ambayo si viongozi wengi hufika. Wakati mwingine
amekuwa anatumia njia za usafiri zinazoogopesha wengi. Hukaka na
wananchi, anakula nao na kufanya nao kazi. Na kubwa zaidi amekuwa anatoa
fursa kwa wananchi kuelezea matatizo yanayowasibu, manung'uniko yao na
kero zao.. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA WA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kinana akihutubia wakati wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa chama
hicho, ambapo alisisitiza kuendeleza utaratibu alionao wa chama hicho
kuwa karibu na wananchi, pamoja na kuisimamia Serikali katika
utekelezaji wa Ilani ya chama hicho.
JK akionesha mfano wa Jembe na Nyundo alama za chama hicho zinazomaanisha kwamba nchi inaongozwa na wafanyakazi na wakulima.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete (katikati)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii maarufu nchini, baada
ya kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama hicho, wakati wa maadhimisho
ya miaka 37 ya CCM, jijini Mbeya
Kinana akiwapiga picha wamiliki wa mitandao ya kijamii (Bloggers)
waliokuwa wakipiga picha ya paoja na Rasi Kikwete baada ya maadhimisho
kumalizika.
Wafuasi wa CCM waliotimiza miaka 37, wakirusha njiwa 37 ikiwa ni ishara ya kuadhimisha miaka 37 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
Msanii Ummy Wenslaus (Dokii), akionesha vimbwanga vyake alipokuwa
akitumbuiza kwa wimbo wake wa CCM wakati wa sherehe za maadhimisho hayo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (kushoto) na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Wilaya ya Rungwe, Richard Kasesera (kulia)
wakicheza ngoma ya ling'oma wakati wa maadhimisho hayo.
Kundi la TOT likiongozwa na Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa likifanya mambo wakati wa maadhimisho hayo
Wasanii wa muziki na filamu wakiwapungia mikono wananchi baada ya kujiunga na CCM leo
Seehemu ya umati wa wananchi ukiwa katika sherehe za maadhimisho hayo
JK akimkabidhi nyaraka mlemavu wa mikono ambayo alimwahidi akiawa ziarani Mbeya siku zilizopita
JK akitimiza ahadi kwa kumkabidhi Bajaji mlaemavu wa miguu
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete (katikati)
akipiga gita alililinunua kwa ajili ya kumpatia msaada msanii (kuia) wa
katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii maarufu nchini, baada ya
kuwakabidhi kadi za kujiunga na chama hicho, wakati wa maadhimisho ya
miaka 37 ya CCM, jijini Mbeya
JK akikabidhi gitaa hilo, iiwa ni kutimiza ahadi aliyomwahidi msanii huyo mwaka jana
Msanii huyo akiwa na furaha baada ya kukabidhiwa gitaa hilo
JK na Kinana wakiwa katika picha ya pamoja na vijana wa vyuo vikuu waliojiunga na chama hicho
No comments:
Post a Comment