Paul
Okoye wa kwanza kulia, akizungumza na waandishi wa habari (hawako
pichani) kuhusu tamasha watakalolifanya kesho Jumamosi. Novemba 23
katika viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni
Peter Okoye ambao kwa pamoja wanaunda kundi la P Square, wakiwa na Mkuu
wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twisa ambao ni
wadhamini wa wasanii hao pamoja na Lady Jay Dee mmoja wa wasanii
watakaowasindikiza jukwaani wasanii hao.
Mkuu
wa Kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule akipeana mkono
na wasanii, Peter na Paul Okoye, maarufu kama P Square wakati
walipowasili kwenda kutoa msaada katika kituo cha watoto wenye ulemavu
wa usonji “Autism” (utindio wa ubongo) cha Msimbazi Mseto, jijini Dar es
Salaam.
.Msanii Peter Okoye akimuweka vizuri katika bembea mmoja
wa wanafunzi wenye ulemavu wa usonji katika shule ya Msimbazi Mseto
jijini Dar es Salaam. Wa kwa nza kutoka kushoto ni mwalimu Mkuu wa shule
hiyo Reuben Gadi na
Mjumbe wa bodi ya shule hiyo Mtumwa Nindi, na wa kwanza kulia ni
mfanyakazi wa Vodacom Tanzania Precious Hughes ambao ni wadhamini
waliofanikisha wasanii hao kutua nchini.
Wasanii wa kundi la P Square (Peter na Paul Okoye) katikati wakimsikiliza Mtoto mwenye ulemavu wa Usonji, Erick
wa shule ya msimbazi Mseto walipokwenda kushiriki kutoa msaada kwa
kituo cha watoto hao. Wa kwanza kushoto ni mwalimu mkuu wa shule hiyo
Reuben Gadi na kulia ni Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni hiyo.
Wasanii wa kundi la P Square wakikabidhi misaada mbalimbali kwa watoto wenye ulemavu wa usonji wa
kituo cha Msimbazi Mseto cha jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni
Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation, Yesaya Mwakifulefule
akishuhudia makabidhiano hayo, na katikati ni walimu wa shule hiyo
wakipokea kwa pamoja misaada hiyo.
Wasanii
Peter na Paul Okoye Maarufu kama P square wakiwa pamoja na Mkuu wa
Kitengo cha huduma za jamii Vodacom Foundation, Yessaya Mwakifulefule
wakicheza pamoja na watoto wenye ulemavu wa usonji wa shule ya msingi ya Msimbazi mseto, wakati waliposhiriki kutoa msaada katika shule hicho kwa watoto hao wenye mahitaji maalum.
========= ======= ==========
· Waviomba kuwapa ushirikiano wasanii wa muziki nchini
· kufanya onesho kwa masaa mawili mfululizo
· Washiriki katika shughuli za kijamii
Baada
ya kuwasili nchini usiku wa jana wanamuziki mapacha Peter na Paul Okoye
maarufu kama “P – Square” wametoa wito kwa vyombo vya habari nchini
kuwasaidia wasanii wandani na kuwa chachu ya mafanikio ya muziki kama
vilivyo vyombo vya nchi nyingine, huku wakiahidi kufanya makubwa katika
Shoo yao ya siku ya leo kwa mashabiki wao watakaojitokeza katika Viwanja
vya Leaders Club.
Wakizungumza
katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hotel ya Hyatt
jijini Dar wasanii hao wamesema wamefurahishwa na mapokezi waliyoyapata
kutoka kwa jamii ya Watanzania na waandaaji wa Tamasha hilo na kuahidi
burudani ya kipekee kwa Watanzania.
Peter
Okoye ambaye ni mdogo wake na Paul alisema, vyombo vya habari vina
mchango mkubwa katika kuwajenga wasanii huku akitoa wito kwa vyombo
hivyo kuwa kichocheo cha kuwajenga wasanii na sio kuwabomoa.
“Vyombo
vya nchini kwetu vimetufikisha hapa tulipo wamejitahidi kutujenga na
kutusaidia kusikika Afrika nzima., Tutaona fahari kama vyombo vya hapa
nchini pia vitajenga uwezo wa kuwasaidia wasanii wa ndani nao waweze
kufika au hata kuzidi hapa tulipo, Tutafurahi siku tukiwaona wasanii
kama kina Jay dee na Ben Pol wakija Nigeria kama sisi tulivyokuja nchini
kwao, alisema Paul.
Paul
Okoye ambaye ni kaka kwa Peter amesema “Tumefurahishwa sana na
mapokezi tuliyoyapata tangu jana usiku hadi kufikia sasa, tumejisikia
faraja kuwa katika nchi hii ya Tanzania watu wake ni wakarimu sana sifa
hizi tumezisikia kwa watu mbalimbali na tumeshuhudia wenyewe tunawaahidi
Mashabiki wetu kufanya Shoo ya uhakika., alisema Paul Okoye.
Kwa
upande wa wadhamini wakuu wa Tamasha hilo Mkuu wa Masoko na Mawasiliano
wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa,alisema wamejisikia faraja kwa
pamoja kufanikiwa kuwaleta wasanii hao ili watoe burudani kwa Watanzania
na kuweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile
kutoa msada wa vyakula katika shule ya Msingi Msimbazi Mseto kwa kupitia
mfuko wa kusaidia jamii wa Vodacom” Vodacom Foundation”.
“Kwa
upande wetu sisi kama waandaaji kila kitu kimekamilika kuanzia, masuala
ya usalama na jukwaa vyote vimekamilika, Pamoja na mambo mengine
tunatoa wito kwa Watanzania kuwai kufika maana onyesho litaanza saa 1 na
kuwa sihii kuwa wastaarabu wakati wote wa Shoo hiyo na kujiepusha na
vitendo vyovyote ambavyo vinaweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Wasanii
kutoka Bongo watakao toa burudani katika Tamasha hilo ni pamoja na
wakongwe, Prof. Jay, Lady Jaydee, Jo Makini”mwamba wa kaskazini”pamoja
na Ben Pol.
Wakati
huo huo wasanii hao na kitengo cha huduma za jamii cha Vodacom
Foundation wameshiriki katika kutoa msaada wa vitu mbalimbali
kwa watoto wenye ulemavu wa akili cha Msimbazi Mseto kilichopo jijini
Dar es Salaam. Huku wakitoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea
kuwasaidia watu wote wasio na uwezo ili kujenga jamii yenye maisha sawa
kwa wote.
No comments:
Post a Comment