GWIJI wa muziki wa dansi mstaafu Muhidin Maalim
Gurumo (pichani) ameugua ghafla mapema leo na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Wajumbe
wa Kamati ya maandalizi ya Tamasha la
Gurumo, Juma Mbizo na Said Mdoe, waliokuwepo Muhimbili, wameiambia Globu
ya Jamii kuwa mwimbaji huyo mkongwe alipatwa na tatizo la shinikizo la
damu na hali
ikawa mbaya kabla ya kukimbizwa hospitalini hapo. Wamesema kwa sasa hali yake inaendelea vizuri na
amelazwa katika wodi ya Mwaisela namba 1.
Wajumbe hao wamesema siku chache zilizopita Gurumo
alikuwa kwenye afya njema na hata siku ya Jumanne alihudhuria kikao cha kamati
hiyo kilichofanyika Vijana Social Hall Kinondoni.
Aidha, wajumbe hao wamedai kuwa kwa mujibu wa
mke wa Gurumo, Bi Pili, ni kwamba hata jana mwimbaji huyo alikuwa hana tatizo
lolote na alifanya mizunguko yake bila ya mikwaruzo yoyote.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha la
Gurumo, Bi Asha Baraka amewataka wapenzi wa muziki kuwa watulivu kwa vile hali
ya mwanamuziki huyo aliyeitumikia fani kwa miaka 53, inaendelea vizuri.
Tamasha la Gurumo limepangwa kufanyika tarehe 14
mwezi ujao katika viwanja vya TCC Club Chang’ombe. Tumuombee dua mzee wetu Gurumo.
No comments:
Post a Comment