Muuguzi katika kituo hicho cha St.
Laurent Diabetes Centre, akimpima Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la
Kilutheri Tanzania (KKKT) Ask. Dk. Alex Malasusa huku Waziri wa Afya na
Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi akishuhudia.
Wananchi mbalimbali wakipata huduma ya kupimwa ugonjwa wa sukari katika kituo hicho cha St. Laurent Diabetes Centre
Burudani kutoka Mjomba Band ikitolewa
******
Ugonjwa
wa Kisukari umekuwa tishio kwa mataifa mengi duniani, Tanzania ikiwemo.
Inasemekana kuwa nchi maskini na zinazoendelea duniani ndio zinazongoza
kwa ugonjwa wa Kisukari. Aidha, kwa sasa ugonjwa wa Kisukari unashika
nafasi ya tatu duniani kueneza vifo.
Katika
makala hii, Mtaalam wa Maradhi ya Kisukari , Dkt. Mary Mayige ,
kutoka kituo cha Kisukari cha St. Laurent Diabetes Centre, jijini Dar es
Salaam anaeleza kwa ufasaha dalili za ugonjwa huu, kinga na tiba yake.
Dkt.
Mary Mayige anafafanua kuwa Kisukari kwa kifupi (na kwa lugha ya
kueleweka) ni ugonjwa unaotokana na kuwa na kiasi kikubwa cha
sukari kwenye damu.
Aliongezea kuwa sukari inapokuwa nyingi kwenye damu ya binadamu, hapo ndipo mtu huyo husumbuliwa na maradhi hayo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kituo cha Kisukari yaani St. Laurent Diabetes Centre,
Dkt. Mary Mayige aliwakaribisha watanzania wote katika upimaji wa bure
wa Kisukari na pressure katika kituo chao kilichopo Msasani karibu na
CCBRT, Dar es Salaam tarehe 10/11/2013. Kabla ya uzinduzi rasmi wa kituo
hicho, watanzania walijitokeza kwa wingi kupima na kujua afya zao siku
hiyo na kujipatia ushauri wa bure kutoka kwa madaktari na wauguzi wa
kituo hicho.
Watu wengi walinufaika na huduma zilizotolewa na kitu hicho cha St.Laurent Diabetes Centre.
Siku
moja kabla ya maadhimisho ya siku ya Kisukari Duniani, kituo cha St.
Laurent Diabetes Centre walifanya uzinduzi rasmi wa kituo chao
Wakiongozwa na mgeni rasmi Mkuu wa Kanisa la KKKT Askofu Dkt. Alex G.
Malasusa, pamoja na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt .Hussein
Mwinyi, na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Mhe. January Makamba
na waheshimiwa wageni waalikwa wawakilishi kutoka serikalini, kwenye sekta binafsi , za umma na sekta za afya.
No comments:
Post a Comment