TAMASHA LA KIMATAIFA LA 32 LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO 2013 LAANZA.
Kiongozi
wa Kundi la Ngoma za asili la Albino Revolution,akiimba moja ya nyimbo
zao za kuhamasisha amani pamoja na kuwaombea watu wenye Ulemavu,wakati
wa Muendelezo wa Tamasha la 32 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni
Bagamoyo,linaloendelea kwenye Ukumbi wa Chuo Kukuu cha Sanaa,Bagamoyo
Mkoani Pwani.Tamasha hilo lilaloonekana kuwa na wapenzi wengi kutoka
sehemu mbali mbali,linatarajiwa kumalizika Septemba 28,2013.
Mmoja wa Wasanii wa Kundi la Ngoma za asili la Albino Revolution akionyesha umahiri wake wa kucheza ngoma hizo kwa namna yake.
Burudani imekolea huku shangwe zikisikika ukumbi mzima.
Umoja ni Nguvu.
Hii namna ya kumaliza burudani kwa Wasanii hawa.
Pichani
ni kivuli cha Msanii wa Maigizo wa Kundi la Mapoloni Cultural Group
aliekuwa akiigiza Jukwaani wakati wa Muendelezo wa Tamasha la 32 la
Kimataifa la Sanaa na Utamaduni,linaloendelea kwenye Ukumbi wa Maonyesho
wa Chuo Kikuu cha Sanaa,Bagamoyo Mkoani Pwani.
Wasanii
wa Maigizo na Ngoma za asili wa Kundi la Mapoloni,wakionyesha umahiri
wao wa kuigiza Jukwaani wakati wa Muendelezo wa Tamasha la 32 la
Kimataifa la Sanaa na Utamaduni,linaloendelea kwenye Ukumbi wa Maonyesho
wa Chuo Kikuu cha Sanaa,Bagamoyo Mkoani Pwani.
Wachezaji wa Ngoma za Asili wakionyesha Umahizi wao jukwaani.
No comments:
Post a Comment