IANPHI KUFANYA MKUTANO WAKE WA 8 TANZANIA.
Kwa
mara ya kwanza katika historia ya Chama cha Kimataifa cha Taasisi za
Kitaifa za afya ya Jamii (IANPHI), Tanzania imepewa heshima ya kuratibu
mkutano wa nane wa mwaka wa taasisi hiyo na kupata nafasi ya
kuing'arisha nchi katika ramani ya dunia na hatimaye kuweza kutangaza
maliasili zake na vivutio vya Utalii vilivyomo. Mkutano huo wa nane wa
IANPHI unataraji kufanyika kuanzia 29 Septemba 2013 hadi 1 Oktoba mwaka
huu jijini Arusha katika Hoteli ya Ngurdoto.
Akizungumza hii leo jijinni Dar es Salaam,
Makamu wa Rais, Chama cha Kimataifa cha Taasisi
za kitaifa za Afya ya Jamii(IANPHI) na Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa
ya
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Dr. Mwele Malecelaamesema
mkutano huo utashirikisha washiriki 150 kutoka nchi 73 wanachama.
Daktari. Mwelecele Malecela ameimabia Father Kidevu Blog,
katika ofisi zake za NIMR jijini Dar es Salaam hii leo kuwa mkutano huo
unataraji kufunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Daktari.
Hussein Mwinyi.
Makamu
huyo wa Rais wa IANPHI Daktari. Mwele amesema kuwa wanachama wa taasisi
hiyo watakao shiriki katika mkutano huo hususan wakuu wa Taasisi za
kitaifa za Afya ya Jamii watapa fursa ya kujadili masuala muhimu ya afya
ya jamii: kugbadilishana uzoefu na kubuni mbinu za kitaalam za
kukabiliana na changamoto zilizopo katika sekta ya afya ya jamii.
"Mkutano
pia utatoa nafasi kwa washiriki kujadili mbinu za kukuza ushirikiano
ili kuimarisha afya ya jamii kuelekea mwaka 2015, ambapo mataifa
yamejiwekea nia ya kukamilisha utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya
milenia (MDG's).
Kauli mbiu katika mkutano huo wa mwaka 2013 ni "Afya ya Jamii baada ya mwaka 2015 na mabadiliko ya majukumu ya Taasisi za kitaifa za afya ya Jamii"
Chama hicho cha IANPHI kina wanachama 81 huku makao makuu ya Sekretarieti yake yakiwa mji wa Helsinki, Finland.
No comments:
Post a Comment