Meli ya Gold Star iiliyosajiliwa
Tanzania ikiwaka moto baada ya mabaharia wake kuichoma iliponaswa ikiwa
imebeba dawa za kulevya aina ya bangi katika pwani ya Italia juzi. Picha
ya Reuters
Kwa mujibu ni kwamba Imesajiliwa
Zanzibar na wakala wa Dubai, mzigo una thamani ya Sh125 bilioni,
mabaharia wajaribu kuichoma moto, wajitosa baharini.
Zanzibar. Jina la Tanzania limechafuliwa tena baada ya meli
ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa nchini kukamatwa ikiwa na tani 30
za dawa za kulevya aina ya bangi zenye thamani ya Pauni za Uingereza 50
milioni (Sh125 bilioni).
Tukio hilo limetokea miezi miwili baada ya Watanzania wawili
kukamatwa na dawa za kulevya zenye uzito wa kilo 150 na thamani ya Sh6
bilioni kwenye Uwanja wa Oliver Tambo, Afrika Kusini.
Habari zilizothibitishwa jana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya
Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA), Abdi Omar zilisema kwamba meli hiyo
ilikamatwa juzi ikiwa na mzigo huo wa bangi.
Alisema baada ya kupokea taarifa za kukamatwa kwa meli hiyo
kutoka kwa Polisi wa Kimataifa (Interpol), ofisi yake iliwasiliana na
wakala wake aliye na ofisi zake Dubai, Falme za Kiarabu, Kampuni ya
Philtex ambayo alisema inafanya kazi ya kusajili meli kwa niaba ya
Serikali na kuthibitisha kuisajili.
Alisema meli hiyo ilisajiliwa mwaka 2011 kwa kazi ya kubeba mizigo chini ya Kampuni ya Gold Star.
Alisema kutokana na tukio hilo, Kampuni ya Gold Star imekiuka
masharti ya Sheria ya Usajili wa Meli na ile ya Umoja wa Mataifa
zinazozuia meli kubeba dawa za kulevya na kuongeza kwamba ofisi yake
itafanya uchunguzi na kuchukua hatua.
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia
Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa alisema naye amesikia kupitia kwenye
mitandao kwamba hajapata taarifa za kina… “Leo ni Jumapili ni ngumu pia
kupata taarifa rasmi kuhusiana na hili.”
“Kesho (leo) tutawasiliana na Polisi wa Kimataifa (Interpol)
ili kufahamu undani wa suala hili. Kuanzia hapo ndipo tutajua nini
kinachoendelea, kama waliokamatwa ni Watanzania au la na hiyo bangi
waliitoa wapi.”
Msemaji wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini
(Sumatra), David Mziray alisema: “Sina taarifa za tukio hilo, labda
tuwasiliane kesho.”
Kama sinema
Taarifa zilizopatikana jana kwenye mitandao mbalimbali ya
kimataifa zinasema meli hiyo ilinaswa maofisa Forodha na askari wa doria
wa Italia waliokuwa Pwani ya Sicily, Bahari ya Mediterania.
Msemaji wa Idara ya Ushuru Italia, alisema: “Meli hiyo
ilikamatwa baada ya kupatikana kwa taarifa za kiitelijensia kuwa imebeba
dawa hizo, lakini hatukutarajia kama kungekuwa na mzigo mkubwa kiasi
hicho na hata wahusika kuipiga moto.
No comments:
Post a Comment