ccm yakipiga jeki kituo cha watoto yatima fema matamba wilayani makete.
Watoto yatima waliopo kwenye kituo cha Fema Matamba.
Katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu akiongea na watoto na walezi wa kituo cha watoto yatima FEMA Matamba.
Katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu akisalimiana na watoto yatima wa kituo cha Fema Matamba.
Katibu akimpa mlezi wa watoto hao misaada hiyo
Sehemu ya misaada iliyotolewa na chama hicho
Muonekano wa kituo cha watoto yatima FEMA Matamba.
==========
Jamii
nchini imetakiwa kujenga desturi ya kusaidia wasiojiweza hasa watoto
waishio katika mazingira hatarishi na wanaolelewa katika vituo vya
watoto yatima kwa kuwa hawakupenda kuishi maisha wanayoishi ya kukosa
wazazi
Rai
hiyo imetolewa hivi karibuni na Katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji
Mtaturu wakati akikabidhi vitu mbalimbali vilivyotolewa na chama hicho
vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 60,000 kwa ajili ya watoto yatima
wanaolelewa katika kituo cha FEMA Matamba kilichopo chini ya KKKT
kilichopo kata ya Matamba wilaya ya Makete mkoani Njombe
Mtaturu
amesema wao kama chama wameguswa na namna watoto hao wanavyoishi katika
kituo hicho kuwa wanahitaji misaada ya kila namna kutoka kwa wanamakete
na ndio maana wamefikia hatua hiyo ambayo wanaimani itaungwa mkono na
watu wengine
"hawa
watoto ni wetu na hakuna anayeweza kuja kutusaidia kuwalea kwa uchungu
kama sisi wenyewe, sisi kama chama cha mapinduzi wilaya ya makete
tumeonesha mfano kwa hiki kidogo tulichokileta tunaomba na wengine
wawasaidie watoto hawa" alisema Mtaturu
Kwa
upande wake askofu Job Mbwilo ameshukuru kwa msaada huo uliotolewa na
CCM wilaya ya Makete na kusema anaimani kuwa wapo wengine
watakaojitokeza kuwaunga mkono hasa ukizingatia kituo hicho hakina mradi
unaokiwezesha kupata fedha zaidi ya kutegemea misaada kwa wajerumani
pamoja na wadau wengie wanaoguswa kuwasaidia kutoka ndani na nje ya nchi
Chama hicho kimetoa sukari, sabuni pamoja na biskuti kwa ajili ya watoto hao
No comments:
Post a Comment