Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia 0712 455 139 au 0687 233 209 wote mnakaribishwa. Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Fast Jet: Imetukomboa, Sasa tunaweza kutumia usafiri wa anga kwa bei nafuu

f1Abiria wa kampuni ya ndege ya fastjet wakipanda dege hiyo kwenye uwanja wa JK. Nyerere wakielekea mkoani Kilimanjaro kampuni hiyo imeanzisha safari za Kilimanjaro- Zanzibar-Kilimanjaro -na kurudi Dar es salaam  f2Ndege ya fastjet inavyoonekana kwa ndani f3Abiria wakiangalia viti vyao tayari kwa kukaa na kuanza safari f4Huduma za vyakula zinaendelea f5Wafanyakazi wa kampuni ya ndege ya fastjet Zanzibar kutoka kulia ni Halima Abdallah,Asedy Ramadhan na Shalifa Nasor wakiwa katika ofisi yao iliyopo uwanja wa ndege wa Abeid Amani Karume Zanzibar f6Marubani wa ndege hiyo kulia ni Captain Tayrol na Lewis f7Marubani wa ndege hiyo kulia ni Captain Tayrol na Lewis wakiwa na Jasmine mhudumu wa ndege hiyo. Kampuni ya ndege ya fastjet imesaidia sana kupunguza gharama katika usafiri wa anga hili limebainishwa na wasafiri wanaotumia ndege za kampuni hiyo katika safari zao huku wakikiri wazi na kusema huu ni ukombozi kwa abiria wenye kipato cha chini.

Pamoja na kuwa ni muda mfupi  sana tangu ilipoanza kufanya kazi  nchini Tanzania lakini ndani ya kipindi hicho kifupi, imeweza kuondoa ile dhana kuwa usafiri wa ndege ni kwa ajili ya watu wenye vipato vya juu.

Faraja Temu  ambaye alisafiri na ndege  hiyo akitokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), akielekea Zanzibar, alimweleza mwandishi wa habari kuwa  “Sasa naweza kupanda ndege, Fast Jet wamerahisha sana maisha ya usafiri.

“Ukiangalia bei ambayo nimelipa, haitofautiani sana na gharama za kawaida za usafiri wa mabasi. Naamini kwamba hivi sasa kila anayesafiri kwa basi, anaweza kupanda ndege na ikawa nafuu zaidi kupitia Fast Jet.” Anachokizungumza Ritha Kabese ni kweli kabisa, kwani mapinduzi ya sasa ya Fast Jet, yanafanya usafiri wa ndege kuwa gharama nafuu mno na kusaidia watu wengi zaidi katika usafiri wa anga Mathalan; kwa usafiri wa basi kwenda Mwanza, nauli ni kati ya shilingi 45,000 mpaka 60,000. Fast Jet yenyewe inatoza nauli ya chini kabisa shilingi 43,000, yaani usafiri shilingi 32,000 na kodi shilingi 11,000, jumla shilingi 43,000.

Vilevile unapopanda Fast Jet, haikulazimu kuingia gharama za ziada kwa ajili ya matumizi ya njiani. Kati ya dakika 45 na 60, unakuwa umeshafika unapokwenda. Hakuna sababu ya kutumia saa nyingi njiani au wakati mwingine kupitisha zaidi ya siku ukisafiri, eti kwa kukimbia gharama za kusafiri kwa ndege, wakati Fast Jet inakusafirisha kwa bei nafuu kuliko hata ile ambayo ungelipa kwa basi.
 
Naye Halima Abdallah mfanyakazi wa Kampuni hiyo kutoka alisema kumekuwepo na chamnagamoto kadhaa katika shughuli zao tangu aingie kampuni ya ndege ya fastjet hasa kwa upande wa mahusiano mazuri na makampuni mengine, ni rahisi sisi kuwaelekeza zilipo ofisi za kampuni zingine kama ndege zetu zimejaa lakini kampuni zingine haziko tayari kutoa ushirikiano huo, hilo ni jambo linaloshangaza kidogo

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...