EPIQ STARS KUWASHA MOTO MAISHA CLUB DAR IJUMAA HII
Ziara
ya kuzindua nyimbo za wasanii walioshiriki shindano la kuimba la Epiq
BSS itaendelea tarehe 1 mwezi wa tatu, ijumaa hii katika ukumbi wa
Maisha Club Dar ambapo wasanii wote walioingia kumi bora wanatarajiwa
kufanya show kali siku hiyo.
‘Pamoja na wimbo wangu wa Siachi pia mashabiki watapata fursa ya kuusikia wimbo wangu utakaoufuata siku hiyo hiyo’ alisema Walter, ambaye alifanya show kali sana Dodoma. Usiku huo pia utapambwa na burudani kali kutoka kwa wakali wengine kama Ben Paul, Barnaba, Linah na Rich Mavoko.
Wasanii hao ambao wiki iliyopita
walifanya show kali katika ukumbi wa Maisha Club Dodoma, wanatarajiwa
pia kufunika Maisha Club. Wasanii hao ambao wengi wamekuwa wakisubiriwa
kwa hamu na wengi tokea shindano lilipoisha mwishoni mwa mwaka jana
wamekuwa wakizungumziwa na wengi kama wanamziki watakaofanya vizuri
mwaka huu. Wasanii
watakaofanya show Dar ni Menina Atick, Nsami Nkwabi, Nshoma, Vincent, Husna Nassor, Geofrey Levis, Wababa Mtuka, Norman Severino pamoja na mshindi wa milioni hamsini, Walter Chillambo.
watakaofanya show Dar ni Menina Atick, Nsami Nkwabi, Nshoma, Vincent, Husna Nassor, Geofrey Levis, Wababa Mtuka, Norman Severino pamoja na mshindi wa milioni hamsini, Walter Chillambo.
Huku baadhi ya nyimbo zikiwa
tayari zinafanya vizuri kwenye soko la muziki kama wimbo mpya wa
Walter-Siachi, Menina-Dream Tonight, Husna-Nawamimina, Wababa-My Wife na
Nsami- Muongo usiku huo pia utakuwa na vitu vipya kibao, pamoja na
uzinduzi wa nyimbo mpya za Norman, Nshoma, Vincent na Godfery.
Akizungumzia show hiyo,mmoja wapo
wa wasanii hao, Walter anasema wapenda burudani wa Dar wasikose kuja
kumshuhudia yeye na wasanii wengine wa Epiq BSS wakifanya vitu vyao
kwani wamejipanga kwa muda mrefu.
‘Pamoja na wimbo wangu wa Siachi pia mashabiki watapata fursa ya kuusikia wimbo wangu utakaoufuata siku hiyo hiyo’ alisema Walter, ambaye alifanya show kali sana Dodoma. Usiku huo pia utapambwa na burudani kali kutoka kwa wakali wengine kama Ben Paul, Barnaba, Linah na Rich Mavoko.
No comments:
Post a Comment