BOATENG, MUNTARI WAFANYA MAUAJI MILAN V BARCELONA
Waghana hatari San Siro, Kevin-Prince Boateng na Sulley Muntari
wakishangilia bao la pili wakati AC Milan ilipoichapa Barcelona mabao
2-0 kwenye dimba la San Siro.
Kevin-Prince Boateng (kushoto) akishangilia bao lakewakati
AC Milan ilipoichapa Barcelona mabao 2-0 kwenye dimba la San Siro, katika mechi ya kwanza ya mtoano wa 16 bora mabingwa Ulaya.
Sulley Muntari akishangilia bao la pili wakati
AC Milan ilipoichapa Barcelona mabao 2-0 kwenye dimba la San Siro jana usiku.
Mpira uliopigwa na Prince Boateng (10) ukienda nyavuni huku mlinda
mlango wa Barcelona, Victor Valdes akiukodolea macho bila ya uwezo wa
kuuzuia.
Furaha ya ushindi; Muntari akishangilia bao lake la dakika ya 81.
Mwanasoka Bora kwa Mwaka wa nne mfululizo, Lionel Messi, akiwajibika
dimbani wakati timu yake ya Barca ilipokubali kichapo cha mabao 2-0
kutoka kwa AC Milan. Licha ya umahiri wake, Messi hakuwa na msaada wa
kuiokoa Barca jana usiku.
Beki wa kati wa Barcelona, Carles Puyol akilalamika katika mchezo huo,
huku akiwa amefunika jraha lake kichwani kwa pamba kuzuia damu
zilizokuwa zikimtoka baada ya kugongana na mchezaji wa Milan.
Kevin-Prince Boateng akifumua shuti na kumbabatiza kiungo Cesc Fabregas aliyelala chini akiugulia kwa maumivu.
Chezea Milan Wewe? Messi (kushoto) na Fabregas (kulia) wa Barcelona,
wakiwa chini - huku wachezaji wa Milan haooo wakichapa mwendo.
Messi akiwa amekaa chini baada ya kuanguka akiwa kwenye mchuano mkali dimbani.
Hakuwa dimbani, lakini alifurahia ushindi wa timu yake akiwa jukwaani
na kidosho. Ni mtukutu Mario Balotelli, ambaye sheria za Uefa
zinamkataza kuichezea Milan katika michuano ya klabu Ulaya msimu huu,
akiwa na mpenzi wake mwanamitindo Fanny Robert Neguesha - wakifurahia
kinachojiri dimbani wakati wa mechi kati ya Milan na Barca.
Mario Balotelli akiwa na mpenzi wake
mwanamitindo Fanny Robert Neguesha wakifuatilia pambano la mabingwa
Ulaya kati ya Milan na Barca - lililoisha kwa Barca kulala kwa mabao
2-0.
No comments:
Post a Comment