Serikali yatakiwa kushirikiana na Sekta binafsi katika kuboresha elimu ya afya juu ya vifaa tiba nchini
Mtaalamu
wa maabara na mshauri wa mashine za mionzi (vifaa tiba ) za binaddamu,
Dk. Pilly Ally akitoa mada katika semina ya mafunzo ya kiafya juu ya
vifaa tiba iliyoandaliwa na Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam jana na
kuhudhuriwa na madaktari mbalimbali kutoka hospitali binafsi na za
Serikali. Kushoto ni Mtaalamu na Mshauri wa Uchunguzi na Utafiti wa
magonjwa ya binadamu wa hospitali hiyo, Dk. Nimish Chhaya.
Baadhi ya Madaktari waliohudhuria semina hiyo, wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zikitolewa kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya TMJ, Dk. Tayabal Jefferji, akizungumza na
waandishi wa habari, Dar es Salaam, wakati wa semina ya mafunzo ya
kiafya juu ya vifaa tiba, iliyoandaliwa na hospitali hiyo jana. Semina
hiyo, ilihudhuriwa na madaktari mbalimbali kutoka hospitali binafsi na
za Serikali za jijini.
Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
SERIKALI
kupitia wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, imetakiwa kutoa ushirikiano
wa moja kwa moja na sekta binafsi ya afya ili kuboresha elimu ya afya
juu ya vifaa tiba kutokana na kukua na kupanuka kwa teknolojia duniani
hali inayopelekea kuzuka kwa uhaba wa vifaa na wataalamu wa kutumia
vifaa hivyo katika kuwahudumia wagonjwa kwa wakati.
Hayo
yamesemwa na madaktari mbalimbali waliohudhuria mafunzo ya elimu ya
afya juu ya uchunguzi, utafiti na kutibia iliyoandaliwa na Hospitali ya
TMJ, jijini Dar es Salaam jana na kujumuisha madaktari kutoka sekta
binafsi ya afya na wengine kutoka katika hospitali za sereikali eneo la
jiji la Dar esSalaam.
Akiongea
na waandishi wa habari waliohudhuria katika semina hiyo, mkurugenzi
mtendaji wa wa Hospitali ya TMJ Dr Tayabal Jefferji amesema kuwa sekta
ya afya inakabiliwa na changamoto nyingi hasa katika nchi zinazoendelea
kutokana na kukua na kupanuka kwa teknolojia ya afya na kupelekea
kubuniwa na kutengezwa kwa vifaa tiba vipya kadri siku zinaposonga mbele
na kuongeza changamoto kubwa kwa watoa huduma za kiafya waliosoma
taaluma hiyo kipindi cha nyuma sana.
“Mimi
nilimaliza elimu yangu ya udaktari mnamo mwaka 1972, wakati huo na leo
karibu ni kipindi kirefu sana ambacho kwa namna moja au nyingine kuna
mabadiliko makubwa sana katika kutoa huduma kwa mgonjwa kwani wakati huo
hata kifaa cha kujifunzia na kupimia magonjwa mbalimbali ilikuwa
microscope ya kuchungulia kwa jicho moja lakini leo tuna vifaa vikubwa
vinavyotumia computer” alisema Jefferji na kuongeza kuwa ni jukumu la
serekali kupitia wizara husika kuendesha mafunzo mbalimbali kupitia
semina ili kutoa fursa kwa madaktari wetu kujifunza mbinu na kanuni
mbalimbali katika kutoa huduma kwa wagonjwa na kukabiliana na changamoto
zinazotokana na mabadiliko ya vifaa tiba, madawa na magonjwa mapya.
Kwa
upande wake mganga mkuu wa Hospitali ya Apolo Medical Centre ilipo
jijini Dar esSalaam Dr. Nazir H Arab amesema kuendesha semina na mafunzo
ya mda mfupi kwa madaktari hapa nchini inaweza kuleta tija na mafanikio
katika sekta ya afya hasa katika utafiti na uchunguzi kwa mgonjwa
lakini mafanikio na mabbadiliko makubwa zaidi ni pale serikali
ikianzisha shule mbalimbali za afya hasa za kuzalisha wataalamu wa
maabara na wataalamu wa upauji pamoja na kuwekeza katika vifaa tiba
adimu na muhimu katika kutoa huduma kwa wagonjwa ili kupunguza sio tu
idadi ya wagonjwa kusafirishwa kwenda kutibiwa nje ya nchi bali pia
kupunguza vifo visivyo vya lazima vinavyotokana na uhaba wa vifaa tiba
au wataalamu.
Naye
Daktari bingwa wa magonjwa ya pua koo na masikia Dr. Emmanuel Ole
Lengine kutoka hospitali ya taifa Muhimbili amesema Tanzania ni moja
kati ya nchi zinazoendelea vizuri katika kuzalisha wataalamu wa afya
katika eneo la Afrika lakini ikibakia kukabiliwa na changamoto ya uhaba
wa vifaa tiba, “ Tanzania ina wataalamu wa kutosha kutoa huduma za afya
lakini vifaa vya kutibia hakuna ndio maana wagonjwa wengi wanapelekwa
kutibiwa nje ya nchi hasa India hali ambayo inaongeza gharama kubwa sana
kwa mgonjwa, ndugu pamoja na taifa kwa ujumla ikiwa ni pamoja na
kuongeza maumivu kwa mgonjwa kwa mda mrefu akisubiri kusafiri.” Alisema
Dr Ole na kuongeza kuwa TMJ inastahili pongezi kubwa kwa kuona kuna
umuhimu wa kuandaa na kuendesha mafunzo kwa madaktari bila kubagua
pamoja na ukweli kuwa Hospitali hiyo ni ya binafsi.
Vifaa
tiba vilivyofundishwa na kuelezewa namna ya ufanyaji kazi wake ni
pamoja na Digital X- Ray ,CT SCANNER na MRI ambavyo kwa pamoja zina
uwezo wa kuona ndani ya nyama laini za binadamu, mifupa, Ubongo, Damu na
sehemu zingine za mwili kwa ukaribu na kutambua tatizo la mgonjwa,
vifaa vyote hivi vinapatikana katika Hospitali ya TMJ ambapo watoa mada
katika semina hiyo alikuwa Daktari mkuu kitengo cha maabara, uchunguzi
na utafiti Dr. Nimish Chhaya kutoka Hospitali ya TMJ na Dr Pilly Ally
mtaalamu wa picha za sehemu za ndani ya mwili Hospitali ya TMJ.
No comments:
Post a Comment