Makamu wa Rais Dk. Bilal asimamia uchaguzi wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Madabida aukwaa Uenyekiti wa Mkoa, Guninita chali
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akiteta jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi Mkuu wa CCM, Mkoa wa Dar es
Salaam, wakati wa mchakato huo wa uchaguzi uliofanyika Ukumbi wa PTA
jijini jana Oktoba 13, 2012.
Mmoja
wa wazee wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, waliohudhuria uchaguzi
huo, akizungumza kusalimia wanachama kabla ya kuanza kwa mchakato huo.
Baadhi
ya wanachama wapiga kura waliohudhuria uchaguzi huo, wakifuatilia
matukio mbalimbali yaliyokuwa yakitokea kwenye uchaguzi huo.
Wagombea
wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, kutoka kushoto
ni Ramadhan Madabida, Chizii na John Guninita, kabla ya kuanza kwa
mchakato wa uchaguzi huo jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akiteta jambo na mmoja wa wasimamizi wa uchaguzi wa CCM, Mkoa wa Dar es
Salaa, Hadija Faraji, wakati wa uchaguzi huo, uliofanyika jana Oktoba
13, 2012, ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiq, akipiga kura kumchagua Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa huo.
Ramadhan Madabida akipiga kura katika uchaguzi huo, uliompatia nafasi ya Uenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam jana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akiteta jambo na Mkurugenzi wa Uchaguzi Mkuu wa CCM, Mkoa wa Dar es
Salaam, wakati wa mchakato huo wa uchaguzi, uliofanyika Ukumbi wa PTA,
Viwanja vya Sabasaba jijini jana Oktoba 13, 2012.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akiteta jambo na Mwenyekiti mpya wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan
Madabida, baada ya Mwenyekiti huyo, kutangazwa rasmi kushika nafasi
hiyo kwa kumshinda mpinzani wake, John Guninita kwa kura 310 kwa 214,
katika uchaguzi uliofanyika jana Oktoba 13, ukumbi wa PTA, jijini Dar es
Salaam.
Wasimamizi wa uchaguzi huo, wakiwa bize kuandaa utaratibu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akimpongeza Mwenyekiti Mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es
Salaam, Ramadhan Madabida, baada ya kuibuka kidedea katika uchaguzi
uliofanyika jana Oktoba 13, 2012 kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba na
kutangazwa mshindi katika kinyang’anyiri hicho, kwa kupata jumla ya kura
310, ambapo alimbwaga mpinzani wake John Guninita, aliyekuwa akitetea
kiti chake, akipata kura 214. (Picha zote na OMR)
Mwenyekiti
mpya wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida (kulia),
akipongezwa na aliyekuwa mgombea mwenzake katika kinyang’anyiro cha
uchaguzi huo, John Guninita, baada ya kutangazwa matokeo na kumsinda kwa
jumla ya kura 310 kwa 214, katika uchaguzi huo, uliofanyika Ukumbi wa
PTA jana Oktoba 13, 2012.
Baadhi ya wanachama wapiga kura waliohudhuria uchaguzi huo.
Mwenyekiti
mpya wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan Madabida, akizungumza
baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi uliofanyika jana Oktoba
13, 2012 ukumbi wa PTA, jijini.
Sehemu ya mashabiki na wanachama wa mgombea Ramadhan Madabida wakishangilia ushindi wa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM, Mkoa wa Dar.
Baadhi
ya mashabiki wa Mwenyekiti mpya wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhan
Madabida na wanachama wa CCM, wakishangilia na kufurahia baada ya
kutangazwa matokeo ya uchaguzi huo, uliompa ushindi wa kiti hicho
kilichokuwa kikikaliwa na aliyekuwa mpinzani wake, John Guninita.
Sehemu ya mashabiki na wanachama wa Madabida wakishangilia ushindi wa Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Dar, Badabida.
Mashabiki
na wanachama wa CCM, wakimsindikiza Mwenyekiti mpya wa CCM, Mkoa wa
Dar, Ramadhan Madabida baada ya kutangazwa mshindi katika kinyang’anyiro
hicho jana.
Mashabiki
na wanachama wa CCM, wakimsindikiza Mwenyekiti wao mpya wa CCM, Mkoa wa
Dar, Ramadhan Madabida baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika
kinyang’anyiro hicho jana.
Mwenyekiti
wa CCM, Mkoa wa Dar es Salaam, aliyemaliza muda wake, John Guninita,
akiondoka ukumbini hapo baada ya matokeo kutangazwa, ambapo aliyekuwa
mpinzani wake, Ramadhan Madabida aliibuka kidedea.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na mwanachama wa CCM, Idd Simba pamoja na baadhi ya wazee
wa Chama hicho.
No comments:
Post a Comment