SUPER SPORT YAITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA KATIKA MEDANI YA MICHEZO KWA KUZINDUA WIKI YA SOKA TANZANIA.
Meneja
Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akitoa ufafanuzi kwa
waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo kuwa Super Sport
wakishirikiana na TFF wapo hapa nchini na kwa mara ya kwanza wanaonyesha
mechi za Ligi ikiwemo timu ambazo hata siku moja hazijawahi kuonekana
kwenye Chaneli ya Super Sport na kuwataka wachezaji wa timu hizo
kuonyesha uwezo wao kwa sababu ni fursa ya pekee kuonekana katika nyanja
ya Kimataifa. Aidha amewataka Watanzania ambao hawajaunganishwa na DStv
wafanye hima kununua ving'amuzi ili waweze kushuhudia mechi hizo pamoja
na chaneli nyinginezo zinazopatikana katika DStv.
Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw.
Peter Fauel akifafanua ujio wa Super Sport nchini Tanzania na
kuipongeza TFF kwa kuonyesha ushirikiano na kuwa Chaneli hiyo itaonyesha
mechi tano za Ligi ya Tanzania kuanzia leo Ijumaa Septemba 28 hadi
Jumatano Oktoba 3 mwaka 2012.
Mkuu wa Super Sport barani Afrika Bw.
Andre Venter akielezea furaha yake kuja Tanzania na kupata fursa ya
kulitangaza soka la Tanzania kimataifa kupitia chaneli ya Super Sport
amesema chaneli hiyo imechafanya kazi katika nchi za Kenya na Uganda na
Sasa ni wakati wa Tanzania kuonyesha kiwango chake cha soka Kimataifa.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa miguu
nchini (TFF) Bw. Leordiga Tenga akitoa nasaha zake wakati wa uzinduzi wa
wiki ya Soka Tanzania ambapo amevitaka vilabu vitakavyopata bahati ya
kuonekana katika chaneli hiyo kuonyesha kiwango cha soka la Tanzania na
kuzingatia nidhamu haswa mechi ya Watani wa Jadi Yanga na Simba ambao
wanatambulika barani Afrika kama timu zenye upinzani mkali.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania
Bi. Furaha Samalu akifurahi jambo na watangazaji wa kipindi cha Africa
Soccer Show wakati wa halfa hiyo.
Meneja Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw.
Peter Fauel akisalimiana na baadhi ya wageni waalikwa katika hafla fupi
ya uzinduzi wa wiki Soka Tanzania iliyofanyika jijini Dar kwenye Hoteli
ya Southern Sun.
Dada Levina kutoka Multichoice Tanzania anayetazama kamera akifurahi jambo na wadau.
Meneja fedha wa Multichoice Tanzania
Bw. Senguti (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice
Tanzania Bw. Peter Fauel.
Baadhi ya Wadau wa michezo wakipata viburidisho wakati wa uzinduzi wa wiki ya soka Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania
Bw. Peter Fauel (katikati) katika tete- a -tete na Rais wa TFF Bw.
Leordiga Tenga na Mkuu wa Super Sport Afrika Bw. Andre Venter.
Mtangazaji wa Jahazi ya CLOUDS FM
Arnold Kayanda (wa pili kulia) na wadau wa tasnia ya michezo wakishow
love mbele ya Camera yetu.
Barbara Kambogi akibadilishana mawazo na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
Crew nzima ya Super Sport iliyotua nchini kwa ajili ya wiki ya Soka Tanzania.
Kipindi cha Africa Soccer Show kwa mara
ya kwanza kilifanyika LIVE nchini Tanzania. Pichani ni Watangazaji
wakifanya mahojiano na Katibu Mkuu wa TFF Bw. Angetile Oseah (katikati).
No comments:
Post a Comment