SIMU YA SAMSUNG YENYE UWEZO WA KUFUKUZA MBU YATUA DAR
Meneja wa Samsung Electronics Tanzania, Kishor Kumar (kushoto) akionesha simu aina ya Samsung Galaxy Pocket Smartphone ya bei nafuu inayouzwa sh. 199,000 ambayo pamoja na kuwa na vitu vingi vilevile ina uwezo wa kuwafukuza mbu. Mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Peter Shadrack (kushoto) akipokea zawadi ya simu kwa niaba ya mwandishi mwenzie wa Channel Ten Ferd Mwanjala aliyeshinda bahati nasibu wakati wa uzinduzi wa simu hiyo.
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Uandishi wa Habari (SJMC), Grace Kijo akionesha kwenye simu hiyo sehemu ambayo ukiweka inaweza kufukuza mbu. PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA
Belinda Lanuo wa mwanafunzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dar es Salaam, akielezea jinsi anavyonufaika na simu hiyo yenye vikorombwezo kibao. |
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala (KIU), akielezea mbele ya wanahabari jinsi simu hiyo inavyomsaidia katika masuala yake ya elimu |
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Uandishi wa Habari (SJMC), Grace Kijo akionesha kwenye simu hiyo sehemu ambayo ukiweka inaweza kufukuza mbu. PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA
SAMSUNG YAZINDUA SIMU MPYA YA SAMSUNG GALAXY POCKET
Dar es Salaam, Alhamisi June 14, 2012:
Kampuni ya SAMSUNG Tanzania leo imezindua rasmi simu yake mpya aina ya Smartphone inayojulikana kama “Samsung Galaxy Pocket”. Uzinduzi huo uliofanyika mbele ya waandishi wa habari jijini leo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, Meneja Mkuu wa Samsung Tanzania Bwana Kishor Kumar alisema, “simu yetu ya Samsung Galaxy Pocket ndio simu ya aina ya Smartphone inayopatikana kwa bei nafuu zaidi kwa sasa hapa Tanzania. Simu hii inampatia mnunuzi thamani halisi ya pesa zake kwani inauzwa kwa shilingi 199,000/= pekee na inakuja ikiwa na offer nyingine nyingi kama simcard na airtel bundle za zawadi”.
Naye Meneja Mauzo na Usambazaji wa kitengo cha Samsung Mobile kwa Tanzania Bwana Sylvester Manyara, aliongeza kwamba “simu zetu za Samsung Galaxy Pocket zitapatikana madukani zikiwa zimeshaunganishwa na offer aina tatu. Offer ya kwanza ni simcard ya mtandao wa airtel, offer ya pili ni Internet bundle ya 250 MB kwa mwezi kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia tarehe ya kwanza ya manunuzi. Offer ya tatu ni SMS 100 kwa mwezi kwa muda wa mwaka mmoja kama ilivyo kwa internet bundle”.
Wakiongea kwa nyakati tofauti baadhi ya wateja walisifia sana simu hii mpya kwa urahisi wa kutumia na Application zake za ajabu. Bwana Gerald Simbo, Mwanachuo wa IFM alisema “Simu hii ina uwezo wa Multi Task yaani inamuwezesha mtumiaji kufanya shughuli zaidi ya nne, hii ina maana unaweza kuwa unaongea na simu, unatumia mtandao wa Facebook nk. Napenda pia uwezo wake wa kuhifadhi miziki kwenye Pocket Music”. Naye Bwana Enock Kweka mwanachuo wa UDSM alisema, “Application ninayoipenda sana mimi ni Find My Mobile, hii inaniwezesha kujua simu yangu ikipotea naweza kuipata wapi, hii ni kwa msaada wa Samsung ambao wanaweza kuiona katika system zao”.
Bi Belinda Lawuo ambaye ni mwanachuo wa CBE alisifia uwezo wa Samsung Galaxy Pocket inavyoweza kufukuza mbu usiku inapowekwa kwa kutumia application yake ya Mosquito Repellant. Bi Grace Kijo, Designer wa mavazi na mwanachuo wa chuo cha SJMC alisema, “Application mpya ambayo iko kwenye simu hii na naipenda ni Swipe, application hii inaokoa muda kwani sina haja ya kuandika neno zima wakati wa kuandika, nagusa tu baadhi ya herufi na neno linajiandika lenyewe mara moja”.
Bwana Manyara alimaliza kwa kusema, “Tunawashukuru watanzania kwa kutuunga mkono kwa muda wote, tumewaletea zawadi hii wafurahie, inapatikana katika maduka yote kwa sasa, tuna matangazo redioni, katika television, mabango ya barabarani na tunawaomba kutembelea website ya simu hii galaxypocket.co.tz na facebook page ya simu hii facebook.com/pages/Samsung-Galaxy-Pocket”.
No comments:
Post a Comment