KINONDONI MABINGWA WA DARTS MKOA WA DAR ES SALAAM 2012
Mwakilishi wa Mauzo wa TBL, Kanda ya Kinondoni, Endrew Misama (kushoto) akiwakabidhi kombe la Ubingwa wa Darts Mkoa wa Dar es Salaa, wachezaji wa timu ya Kinondoni.
TIMU ya Kinondoni ya wanaume imefanikiwa kutetea ubingwa wa mashindano ya Darts 'Vishale' Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Moshi jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo yaliyojulikana kama 'Dar es Salaam Darts Association Tournament 2012', yalidhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) upitia kinywaji chake cha Safari Lager.
Kinondoni imechukua ubingwa wa mashindano hayo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuzishinda timu za Ilala na Temeke zilizoshiriki mashindano hayo.
Kwa timu ya wanaume washindi ni Kinondoni pointi 10 wamepewe zawadi ya Shilingi laki tatu na kombe kubwa.
Washindi wa pili ni Ilala baada ya kuibuka na pointi nane ambao waliondoka na kikita cha shilingi laki mbili na Temeke walikuwa washindi wa tatu katika mashindano hayo, baada ya kupata pointi sita na walizawadiwa shilingi laki moja.
Kwa upande wa timu ya wanawake washindi ni Ilala baada ya kupata pointi tano, Temeke walishika nafasi ya pili walioshinda pointi tatu na Kinondoni waliambulia patupu.
Washindi wawili wawili wanaume ni Alikhani Wallni, Bakeshi Salonk, Uwari Habib na John Hezroni, kwa upande wa wanawake ni Iren Kihupi.
Mashindano hayo yaliandaliwa na Chama cha Darts Mkoa wa Dar es Salaam (Dada), yalishirikisha timu za zilizo katika wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni za wanaume na wanawake.
Katika mashindano hayo pia yalishirikisha wachezaji binafsi, mmoja mmoja na wachezaji wawili wawili na washindi waliondoka na zawadi iliyotolewa na wadhamini hao.
Mgeni rasmi alikuwa ni mwakilishi wa Mauzo wa TBL, Kanda ya Kinondoni, Endrew Misama.
No comments:
Post a Comment