Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia 0712 455 139 au 0687 233 209 wote mnakaribishwa. Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Tukio zima la Ajali mbaya la basi la Prince Muro iliyo tokea jana Usiku maeneo ya Senjele likielekea Tunduma. Mwendo kasi ndio chanzo cha ajali hiyo mmoja Afariki 14 majeruhi

Basi la Price Muro Baada ya kupata ajali usiku wa kuamkia jana likielekea Tunduma kutokea Dar es salaam.

Likiwa linaonekana baada ya kupinduka

Hivi ndivyo zinavyo onekana Damu na viti kuharibika vibaya baada ya ajali hiyo iliyo tokea jana usiku

Baadhi ya mabaki ya vitu baada ya ajali hiyo jana usiku

Hili Ndilo Gari la mizigo ambalo basi la Price muro lilitaka kulipita, na baadae kushindwa na kupinduka baada ya kukutana na Gari lengine mbele yake


Shimo hili limechimbika wakati wa ajali hiyo ilipo tokea jana usiku

Hapa ndipo Basi la Prince Muro lilipo taka kuingia na kulikwepa gari hili na kupindukia upande wa pili

Muonekano wa gari hili la mizigo ambalo limeharibikia bara barani

Mmoja wa majeruhi ambae alikuwa anatokea Dar es salaam kwenda kuwasalimu ndugu zake Ileje aliye fahamika kwa jina moja tuu la Andendekisye akiwa katika Hospital ya Ifisi Mbeya Muda huu

Baadhi ya Majeruhi walio nusurika katika ajali hiyo wakiwa katika Hospitali ya Ifisi kuelekea katika matibabu na kutazamwa kama wamepata matatizo yoyote.

Hawa ni majeruhi kati ya wale 14

Mganga mkuu wa Hospitali ya Ifisi Dkt. Mbilinyi akiongea na moja ya majeruhi mapema leo.

Majeruhi ambao wamenusurika katika ajali hiyo mbaya wamesema kwamba dereva huyo alikuwa mwendo kasi tangia walipo fika mikumi, Wameendelea kudai kwamba walimpa onyo mala kadhaa lakini hakuweza kuwasikiliza na akaongeza mwendo kasi zaidi mpaka walipo pata ajali hiyo maeneo ya Senjele kuelekea Tunduma.
Habari kamili itakuja mpaka sasa kuna majeruhi 14 na mtu mmoja amefariki Dunia. (chanzo; kamanda wa matukio Blog).

1 comment:

crispaseve said...

aisee hii ajali ni mbaya sana na inaonekana kwa mwaka huu kidogo zimekuwa chache

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...