Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia 0712 455 139 au 0687 233 209 wote mnakaribishwa. Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

PRECISION AIR YAZINDUA SAFARI ZA KWENDA AFRIKA KUSINI MARA NNE KWA WIKI!

Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya ndege ya Precision Air Michael Shirima akitoa maelezo wakati wa uzinduzi wa safari ya kwanza ya Ndege ya kampuni hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 111, ambayo imeanza safari yake kati ya Dar es Salaam kwenda Johannesburg Afrika Kusini wakati wa hafla hiyo iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jana.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Alfonse Kioko na (Kushoto) Mkurugenzi wa TCAA John Njawa.
Mkurugenzi Mkuu na Meneja Mwendeshaji wa Precision Air Alfonse Kiako,(katikati) Mkurugenzi wa Biashara Phil Mwakitawa (kulia) na Meneja Mauzo Tuntufye Mwambusi wakiwa uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere wakisubiri kuzinduliwa kwa safari ya kwanza ya Ndege ya kampuni hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Johannesburg Afrika kusini jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Precision Air Michael Shirima (kushoto) akitoa maelezo kwa abiria waliokuwa wakisafiri kwenda Johannesburg wakati wa uzinduzi wa safari ya kwanza ndege ya kampuni hiyo kutoka Dar es Salaam kwenda Johannesburg Afrika kusini, hafla hiyo ilifanyika jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Baadhi ya abiria wakisubiri kusafiri na Ndege nambari PW 700.Boeing 737-300 ya Shirika la ndege la Precision Air ambayo ilizindua safari yake jana kati ya Dar es Salaam kwenda Johannesburg Afrika Kusini, kwa promosheni ya Dola 57 ili kuwawezesha watu wengi kusafri na shirika hilo.
Baadhi ya Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakisubiri kusafiri na Ndege nambari PW 700 Boeing 737-300 ya Shirika la ndege la Precision Air ambayo ilizindua safari yake ya kwenda Johannesburg Afrika Kusini jana kwa promosheni ya Dola 57 ili kuwawezesha watu wengi kusafiri na shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Ndege la Precision Air Michael Shirima wa pili kushoto, Mkurugenzi wa TCAA John Njawa, Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi, Wizara ya Uchukuzi, William Nshama (kulia) na Mkurugenzi wa Biashara Phill Mwakitawa wakijadilia jambo katika hafla ya uzinduzi wa safari ya ndege ya Precision Air kwenda Johannesburg Afrika Kusini kwa promosheni ya Dola 57

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...