Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia 0712 455 139 au 0687 233 209 wote mnakaribishwa. Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

NAPE AKAGUA CHUO CHA CCM CHA IHEMI MKOANI IRINGA LEO.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, leo amefanya ziara kukagua mradi wa kufufua chuo cha CCM cha Ihemi, mkoani Iringa. Pichani, Nape akiwa katika matukio mbalimbali. PICHANI: Msimamizi wa shughuli za ufufuaji Chuo Cha Chama Ihema mkoani Iringa, Simon Nchimba (wa nne kulia) na Nape ( watano kulia) wakitazama eneo la chuo hicho. Picha zote na Bashir Nkoromo

Msimamizi wa Chuo Cha Ihemi Simon  Nchimba  (kulia) akimuonyesha Nape kisima cha maji kilichopo chuoni hapo chenye urefu wa futi saba.

Nape na Simon Nchimba wakiwa kwenye moja ya vitanda vilivyoko kwenye mabweni ya chuo cha Ihemi.

Msimamizi wa Chuo cha Ihemi mkoani Iringa,  Simon Nchimba akimpa maelezo Nape kuhusu maendeleo na changamoto zinazokabili ufufuaji wa chuo hicho. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa huo, Deo Sanga  'Jah People'.

Nape akikagua mashine ya kukata ubao, katika  chuo cha Ihemi, mkoani Iringa. Wapili kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Iringa  Emmanuel Mteming'ombe na maofisa wengine wa Chama.

Nape akiwa kwenye banda la mamalishe lililopo njiapanda ya Chuo cha Ihemi na Barabara kuu mkoani Iringa, ambapo alizungumza na mamalishe huyo (kulia) kuhusu changamoto zinazomkuta katika biashara zake.

Nape akimpa bendera ya CCM, mwananchi aliyeng'ang'ania kupewa bendera hiyo, msafara wa Nape ulipopita eneo la njia panda ya Chuo cha Ihemi.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...