MAJALIWA: Jitokezeni kwa wingi siku ya sensa
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Kassim Majaliwa (kulia), akimkabidhi katiba Diwani wa Kata ya Mandawa,Rajab Lipei katika hafla iliyofanyika, Ruangwa mkoani Lindi hivi karibuni.
WANANCHI wa wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi wametakiwa kutojifungia vyumbani wala kujificha mashambani na badala yake wajitokeze kwa wingi ili waweze kushiriki kikamilifu kwa kutoa taarifa sahihi siku ya sensa wa watu itakayofanyika Agosti 26 mwaka huu.
Imeelezwa kuwa iwapo wananchi hao watashiriki kwa wingi na kutoa taarifa sahihi kwa maofisa wa watakaofika majumbani kwao kwa ajili ya kuwahesabu, itasaidia katika kuboresha maendeleo yao.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Mandawa hivi karibuni, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), anayeshughulikia Elimu, Kassim Majaliwa alisema ni lazima wajitokeze kwa wingi na wahesabiwe kwani bila ya kuwa na idadi sahihi ya watu katika eneo husika ni vigumu kupata maendeleo.
Majaliwa ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa alisema sensa inasaidia kupata idadi kamili ya watu walio kwenye eneo husika hivyo hata mafungu ya fedha yanayotolewa na serikali kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo yatoka kulingana na idadi ya watu hivyo ni lazima wahesabiwe kwa ajili ya maendeleo yao.
"Ruangwa tupo wengi lakini takwimu zinaonekana hatuzidi watu laki mbili jambo ambalo si sahihi ni lazima tukahesabiwe kwani misaada tunayoipata ni ya watu wachache kulingana na takwimu za miaka ya nyuma na sasa tumeongezeka hivyo hatuna budi kuhesabiwa kwa ajili ya maendeleo yetu.
Pia kuhesabiwa kwenyewe wala hakuchukui muda mwingi labda tukasahindwa kwenda shambanii walaa, mchakato wenyewe ni wa muda mchache kwa kuwa mchakato huo unafanywa na watu wengi hivyo siku ikifika kama huna safari ya dhalura ni lazima uhesabiwe kwanza ndipo uondoke na hata kama utakwenda kulala mbali na nyumbani utahesabiwa tu kwani maofisa watapika kote hadi gesti," alisema.
Katika hatua nyingine aliwataka wananchi hao kushiri kutoa maoni pindi tume ya mabadiliko ya katiba itakapofika katika maeneo yao na wasikubali kushawishiwa na watu kutoa maoni ya kuchaguliwa.
Alisema kuna baadhi ya watu wanataka kuwapotosha wananchi kwa kuwapangia mambo ya kuchangia wakati wa kutoa maoni ya mabadiliko ya katiba jambo ambalo si sahihi kwani kila mwananchi anatakiwa kutoa maoni yake binafsi.
"Nawaomba ndugu zangu msikubali kupotoshwa na watu ambao hawajui hata rangi ya katiba ambao wanapita katika maeneo yenu na kuanza kuwapangia maneno ya kuzungumza wakati wajumbe wa tume ya marekebisho ya katiba watakapika, msikubali kila mtu anatakiwa kuwa huru na kutoa maoni ambayo anaona yatasaidia kuboresha maendeleo au kutatua kero yake ndani ya katiba," alisema.
Katika kuhakikisha wananchi wanasoma na kuielewa vizuri katiba ya zamani ambayo inatakiwa kufanyiwa maboresho. Majaliwa aligawa nakala 400 za katiba hiyo kwa viongozi mbalimbali wa Chama na serikali na kuvigawa katika ofisi mbalimbali ambazo wananchi watapa fursa ya kuisoma na kuielewa ili waweze kutoa maoni yao kwa ufasaha wajumbe wa tume watakapofika katika maeneo yao.

No comments:
Post a Comment