Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia 0712 455 139 au 0687 233 209 wote mnakaribishwa. Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

Advertise your Business here at very cheap price Contact us through +255 712 455 139 or +255 687 233 209 your all welcome.

KATIBU CCM, NORTH LONDON AGOMBEA NEC,UWT, TAIFA

 Mkuu wa Idara ya Oganizesheni na Siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma (kulia) akimkabidhi fomu ya kugombea nafasi ya NEC na Uwakilishi wa UWT Taifa, Neema Kumba.
 Neema Kumba.
Na Andrew Chale

KADA  wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia umoja wa vijana wa (UVCCM) na Msomi wa  digrii ya uchumi, Neema Kumba amejitosa kwenye uchaguzi mkuu wa umoja huo Taifa kwa kuchukua kugombea nafasi ya NEC na uwakilishi UWT.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, muda mfupi baada ya kukabidhiwa fomu hiyo na Mkuu wa Idara ya Oganizesheni na siasa UVCCM, Taifa, Sophia Duma,

Kumba ambae awali alikua Katibu wa CCM, tawi la North London, Nchini Uingereza,alipokua akichukulia digrii yake ya uchumi, alisema lengo ni kuakikisha mikakati thabiti  inajengeka kwa  kiwango kikubwa miongoni mwa vjana na wanawake wote nchini.

“Kwa umakini wangu na maarifa niliyoyapata kwenye elimu na uwepo wangu ndani ya chama, ndani na nje ya nchi, ni wakati sasa na mimi kuwasaidia wenzangu hasa Vijana na wanawake ambao mara nyingi wamekua wakisahauriwa  na huu ndio wakati wa kuwainua” alisema Kumba.

Mbali na kuchukua fomu hiyo ya NEC na uwakilishi UWT, Taifa, pia tayari alisha chukua fomu ya kuwania nafasi ya Mwenyekiti Uvccm, Wilaya Ilala.

Mpaka sasa tayari wanachama mbalimbali wa UVCCM, wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi ambapo mwisho wa kurudisha fomu hizo, Agosti 6.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...